LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 6, 2016

BENKI YA BancABC YATOA OFA KWA WATEJA WANAOFUNGUA AKAUNTI YA AMANA MSIMU HUU WA SIKUKUU

Dar es Salaam, TANZANIA
Wateja wa Benki ya BancABC wanaofungua akaunti ya amana kwa kuweka fedha kuanzia sh. milioni kumi kwa muda maalum katika msimu huu wa sikukuu watanufaika zaidi kwa kupata riba ya juu kuliko zote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na wafanya biashara wadogo, Joyce Malai, alisema katika ofa hiyo ambayo iilianza jana, Desemba 5, 2016, BancABC, inatoa riba ya hadi asilimia 16, kwa mwaka na wateja watalipwa riba hiyo papo kwa papo ikiwa ni zawadi yao msimu huu wa sikuku.

“Hii ni ofa bora kuliko zote kwenye soko kwa sasa na tunataka kuwashawishi wateja wetu na hata wale wasiokuwa na akaunti kwetu kutumia fursa ya ofa hii ya msimu huu wa sikukuu,” alisema Joyce.

Alisema,  Benki ya ABC ambayo ni sehemu ya  Atlas Mara,  ina nia ya kufikia mahitaji ya wateja na kuhakikisha kwamba wanakua pamoja na benki hiyo. “Tunathamini jinsi wateja wetu wanavyotuunga mkono na hiyo ndio sababu sisi kama benki tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe katika msimu huu wa sikukuu.” alisema.

“Kinachotakiwa kufanywa na mteja yeyote ili aweze kujipatia ofa hii nikufika kwenye tawi letu lolote , Uhuru, Quality Centre, Kariakoo na Arusha, na kufungua akaunti ya amana ya muda maalumu, na kwa kweli riba hiyo italipwa papo hapo, lengo ni kumpa mteja uhuru wa kuitumia riba hii kwa ajili ya kufanya manunuzi  binafsi kama apendavyo ikiwemo kununua zawadi kwa familia au marafiki ili kuwaongezea furaha katika msimu huu wa sikukuu,” alisema.

Aliendelea kusema kwamba ofa hiyo itawahusu wateja watakaofungua akaunti za amana za muda maalumu katika Benki hiyo kabla ya Desemba 31, mwaka huu, akimaanisha kwamba ofa hiyo itakuwa halali kwa msimu wa sikukuu tu.

“Tunataka msimu huu wa sikukuu kuwa mzuri zaidi kwa wateja wetu kwa kuwa tunafahamu kwamba watu wengi hutumia kiasi kikubwa cha fedha wakati wa Krismasi. Kupitia riba hii watakayopata awali, wataweza kupata mahitaji yao kirahisi,” alisema.
Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo, na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogo wadogo, Joyce Malai (kulia), wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu Benki hiyo kuzindula ofa ya riba inayolipwa papo kwa papo ya asilimia 16 kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya muda maalum msimu huu wa sikukuu. Walizungumza na wandishi hao makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages