Balozi wa Russia nchini Uturuki amepigwa
risasi na kuaga duani kwa majeraha baada ya kumiminiwa risasi wakati
alipokuwa akihutubia kwenye maonyesho ya katika mji mkuu wa nchi hiyo
Ankara.
Ripoti zinasema kuwa, balozi Andrey Karlov alishambuliwa kwa
risasi katika eneo la sanaa ya uchoraji katika mji mkuu wa Ankara
yaliyodhaminiwa na ubalozi wa Russia mjini humo. Taarifa za awali
zinasema kwamba, balozi huyo alikuwa akitoa hotuba wakati mtu aliyekuwa
aliyekuwa na bunduki alipompiga risasi na kutoa ujumbe kwa lugha ya
Kirusi.
Watu kadhaa wamejeruhiwa katika tukio hilo la kigaidi ambapo picha za
tukio hilo zimewaonyesha watu wawili waliovalia nadhifu wakiwa wamelala
chini ,karibu na kipaza sauti. Mshambuliaji huyo alisikika akitoa
maneno kwa lugha ya Kirusi na kubandua baadhi ya picha zilizokuwa katika
kuta za maonyesho hayo.
Maria Zakharova, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Russia amethibitisha habari ya kufariki dunia balozi huyo.
Serikali ya Russia imelaani vikali shambulio hilo na kulitaja kuwa ni
la kigaidi.
Vyombo vya usalama vya Uturuki vimesema kuwa, mtekelezaji wa shambulio hilo alikuwa afisa polisi anayefanya kazi katika mji wa Ankara. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, maafisa wa polisi walifanikiwa kumpiga risasi mtekelezaji wa shambulio hilo na kumjeruhi vibaya huku baadhi ya ripoti zikisema ameuawa katika shambulio hilo la maafisa usalama.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇