MAHAFALI YA TISAYA CHUO CHA
KODI
Chuo cha Kodi kinapenda
kuwatangazia wahitimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 na Umma kwa ujumla kuwa
Mahafali ya Tisa (9) yatafanyika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jumamosi tarehe 17 Desemba, 2016, kuanzia saa Tatu asubuhi. Katika mahafali
hayo wahitimu wa programu zifuatazo watatunukiwa astashahada, stashada na
shahada:
1. Cheti Cha Uwakala wa
Forodha cha Afrika Mashariki(CFFPC)
2. Stashahada ya Usimamizi Wa
Forodha na Kodi (DCTM)
3. Shahada Ya Usimamizi wa
Forodha na Kodi (BCTM
4. Astashahada ya Uzamili ya
Uongozi wa Forodha ya Africa Mashariki (PGCCA)
5. Stashahada Ya Uzamili
Katika Kodi (PGDT)
Wahitimu wote wanaopenda
kushiriki wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Kuthibitisha kabla ya
tarehe 8/12/2016, kwa Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala kwa
maandishi kuwa watashiriki.
2. Kulipia kiasi cha shilingi
50,000 kwa ajili ya joho na kuwasilisha stakabadhi ya malipo kwa Makamu Mkuu wa
Chuo kabla ya 8/12/2016. Malipo yote yafanyike kupitia Benki ya CRDB, Akaunti
ITA Fee Collection Account No. 0150303205600.
3. Wahitimu waliolipia
watachukua majoho na kuhudhuria mazoezi Ukumbini siku ya Ijumaa tarehe
16/12/2016, saa 3.00 asubuhi.
Wahitimu watakaoshiriki
watagharimia usafiri na malazi yao kwa kipindi chote watakapokuwa Dar es Salaam
kwa ajili ya mahafali.
Tafadhali mjulishe na
mwingine.
Wote mnakaribishwa
Imetolwana:
Mkuuwa Chuo,
ChuochaKodi
Eneo la
Viwanda MIKOCHENI "B",
S. L. P.
9321, Dar es Salaam.
Simu:
+255 22 2925100
Baruapepe:ita@tra.go.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇