MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MH. JOHN KAYOMBO
Na Nassir Bakari
Hatua ya Mkurugenzi kutembelea hapo imekuja
muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi
jirani na kiwanda hiko.
Mkazi mmoja anayefanya biashara karibu na
eneo hilo amesema muda mrefu wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi,
wakaamua kumfikishia kiongozi shupavu, mwenye nia ya dhati ya kuwatumukia
wananchi Mh. John Kayombo.
Baada ya malalamikio ya wananchi kumfikia,
bila kupepesa macho Mkurugenzi Kayombo
akaenda New House Corporation bila kutoa
taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa nia ya kwenda kuona hali halisi.
Baada ya kuona hali hiyo Mkurugenzi Kayombo
alisema sio vizuri kuona binadamu tukitesana wenyewe kwa namna mbalimbali .
“Hii hali ikiendelea itasababisha
wafanyakazi wengi kupoteza uwezo wa kusikia hatimaye kushindwa kufanya kazi za
kujenga Taifa,” alisema Mkurugenzi Kayombo.
Pia Mkurugenzi Kayombo alisema Kiwanda hicho
kujitadhimini katika utendaji wa kazi na kuhakikisha wanapunguza ama kuondoa
kabisa kelele zinazotolewa na mashine hiyo.
Ziara ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Mh. John Kayombo imefichua mambo mengi likiwemo kelele
zisizo za kawaida zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni
ya New Habari Corporation zinazohatarisha uwezo wa kusikia wa wafanyakazi.
Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi Kayombo
alikagua maeneo mbalimbali yanazonguka kiwanda na hatimaye akafika kwenye
mashine ya kutengeneza magazeti yanayotolewa na kampuni hiyo .
Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali
ambayo sio rahisi kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi
wakiwa hapo tena bila kifaa chochote cha kuzuia ama kupunguza sauti hizo.
“Hili jambo sio zuri, haiwezekani mashine
ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti, huu ni
ukatili na ni kwenda kinyume na haki za binadamu,” alisema Mkurugenzi na
kuendelea:-
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇