Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani
Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wakikagua Ujenzi wa
Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala wilaya mpya ya Kibiti.
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani
Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wamefanya Ziara ya
Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala lililopo
Wilaya Mpya ya Kibiti na kukabidhi kiasi cha milioni moja 1.000.000/=
huku shilingi milioni Nne na elfu Hamsini zikiwa zimeingizwa kwenye
akaunti na kufanya jumla ya fedha ya mchango walioutoa katika ujenzi wa
daraja hilo kufikia shilingi Milioni Tano na Elfu Hamsini 5.050.000/=.
Msaada huu unafuatia Ahadi iliyotolewa
na Wabunge hao wakati wa Kampeni katika kusaidia Wananchi wa Maeneo ya
vijiji hivyo ambao kwa sasa wanatumia Daraja la Muda lililojengwa kwa
miti na wananchi wenyewe ili kuwawezesha Kuvuka mto.
Ni muda mrefu sasa hawana daraja ambapo
kipindi cha mvua Maji hujaa na kuwapa shida wananchi hasa Kina Mama
Wajawazito na Wanafunzi hushindwa Kuvuka na baadhi yao wamepoteza
Maisha kwa kusombwa na maji kutokana na tatizo la kukosekana kwa Daraja
hilo.
Bajeti ya Ujenzi wa Daraja hilo
imefika Milioni Kumi ambapo wabunge hao wamewashukuru Wadau wote
waliowaunga Mkono katika kutimiza Ahadi hii ya kusaidia Wananchi
wa Vijiji takriban saba hususan Kina Mama Wajawazito na Wanafunzi
ili kuvuka usalama wanapokwenda Kupata huduma mbalimbali zikiwemo
Afya na Elimu.
Wabunge hao waliwaomba wadau mbalimbali
walioahidi kuchangia ujenzi wa daraja hilo katika Kata Mbili za
Maparoni na Msala na Wilaya ya Mafia kukamilisha ahadi zao mungu
awajaalie wafanikiwe kupata chochote ili waweze kuchangia ili tuweze
kukamilisha ujenzi huo ambapo bado unahitaji shilingi milioni 5.000.000
zingine ili kukamilisha bajeti ya ujenzi wa daraja hilo ambayo ni
shilingi milioni kumi 10,000.000.
"Tunaamini mtakapo pata fursa
Mtachangia Mwenyezi Mungu Awawezeshe Amiin" Alisema Mh. Subila Mgalu
huku akimaliza kwa kuwashukuru Viongozi wa Chama, Jumuiya zake ,
Serikali Ngazi ya Wilaya na Kata kwa mashirikiano makubwa na mapokezi
Mazuri.
Daraja litakapokamilika litasaidia
Vijiji Saba Kipoka , Usimbe ,Maparoni ,Msala ,Twasalie ,Kihasi ,Kiechuru
,Kibanjo Kata Tatu na pia Njia hii inatumiwa Kufika mpaka Mafia. ambapo
kwa sasa kumekuwa na athari yingi hasa kwa akina Mama wengi wajawazito
wanashindwa kuvuka Maji yanapojaa na kupelekea kujifungua Njiani.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani
Subira Khamis Mgalu akifurahia jambo wakati wa Ziara ya Kukagua
Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani
Subira Khamis Mgalu wakionyeshwa vipimo vya daraja na wananchi wakati
wa Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akiwa amekaa na wakina mama wakati wa ziara hiyo wilaya mpya ya Kibiti
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani
Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wakikabidhi fedha taslimu
shilingi milioni moja kwa kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja la Usimbe
-Maparoni - Msala wilaya mpya ya Kibiti.
Hali ya Vyombo vya Usafiri waliyoikuta
wabunge hao wakati walipofanya ziara Mwaka Jana 3/10/2015 ambayo
iliwagusa na kuwahamasisha kutafuta Michango ya ujenzi wa daraja
hilo Daraja
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇