Mhandishi James Mtayakingi Kilaba |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi James Mitayakingi Kilaba kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na kusambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dar es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi James Mitayakingi Kilaba umeanza jana, Jumamosi, Oktoba 8, 2016.
Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba alikuwa akikaimu nafasi hiyo, baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk. Ally Yahaya Simba kutenguliwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇