Mfalme
Mohammed VI wa Morocco akishuka kwenye ndege iliyomleta akiwa
ameongozana na ujumbe wake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) jijini Dar es salaam
leo Oktoba 23, 2016
Mfalme
huyo amepokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli jioni hii, Mfalme Mohammed VI
atakuwa nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu.
(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mfalme Mohammed VI wa Morocco akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA leo jioni.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana
na mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam jioni hii.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akielekea
karibu na ndege iliyomleta mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara
baada ya kuwasili jijini Dar es salaam.
Mfalme
Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akiwa ameongozana na Mwenyeji
wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe
Magufuli.
Mfalme
Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP
Ernest Mangu huku akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli
akimtambulisha Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Dk. Modestus Kipilimba
kwa Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakati alipowasili jijini Dar es
salaam leo.
Mfalme
Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza
Kamishna John Casmir Minja huku akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akiongozana
na Mwenyeji wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa JNIAleo jioni.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akiangalia
vikundi vya ngoma na Mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakati
alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.
Mfalme
Mohammed VI wa Morocco akipungia mkono wananchi waliojitokeza kumlaki
huku akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dk. John Pombe Magufuli.
Ndege iliyomleta Mfalme Mohammed VI wa Morocco ikiwasili.
Ndege iliyomleta Mfalme Mohammed VI wa Morocco ikijiandaa kutua kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumlaki Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakati alipowasili jijini Dar es salaam .
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇