LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 17, 2016

WAZIRI NAPE AAHIDI KUTOA SHILINGI LAKI TANO KWA KILA GOLI LITAKALO FUNGWA NA SEREGETI BOYS KESHO

NAPE NNAUYE
Na Lorietha Laurence-
WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa sh. 500,000/= kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Serengeti Boys  katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, dhidi ya Congo-Brazzaville.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Nape amesema milango ipo wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea katika kuiwezesha timu  na hivyo kufanya vizuri katika  mechi hii ambayo ni muhimu sana kushinda ili kufuzu kwa fainali hizo.

“Hii timu ni yetu sote hivyo inahitajika tuimiliki, tuepe nguvu, tuiombee ili iweze kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia fainali kwa kuitoa timu ya Congo-Brazzaville” alisema Nape.

Aidha aliongeza kuwa kesho asubuhi atakutana na wachezaji wa timu hiyo ili kuwapa maneno ya faraja kabla ya kuanza kwa mechi na kuwataka watanzania  kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa motisha wachezaji kwa kuwashangilia  na kuwatia moyo.

Mbali na hayo Waziri Nape alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya kadi za kieletroniki zilizozinduliwa hivi karibuni kwa kueleza kuwa kadi hizo bado hazijaanza kutumika rasmi ili zitaanza kutumiwa katika mchezo baina ya Wabunge wa Simba na Yanga pamoja na Bongo Fleva.

Timu ya Serengeti Boys inaundwa na vijana wa Kitanzania wenye umri chini ya miaka 17 ambapo katika mchezo wa kesho watahitaji ushindi na baadaye kufanya mechi ya marudiano mnamo Oktoba 2 mwaka huu nchini Congo-Brazzaville.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages