Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix
Michel.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk.
Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa
Shelisheli, Alix Michel
Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk.
Augustine Mahiga nchini Shelisheli.
Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya
pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani
ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Tanzania
ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama
ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36
wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31
Agosti, 2016.
Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt.
Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa
Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza
ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8
- 10 Septemba, 2016.
Wajibu huu
wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na
misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa
nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa
niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na
waangalizi kutoka nchi za SADC .
Wakati
akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na
kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix Michel Rais wa Sheliseli .
Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel
Morgan, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Seychels na kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.
Imetolewa na :
BALOZI INNOCENT E SHIYO
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇