Mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo jijini Mwanza.
Na Nassir Bakari
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka
Mkandarasi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Group
anayejenga uwanja wa ndege wa Mwanza kumaliza kazi ya upanuzi wa uwanja
huo ifikapo mwezi Februari Mwakani.
Profesa
Mbarawa ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua kazi ya ujenzi na upanuzi
wa uwanja wa ndege wa Mwanza pamoja na daraja la watembea kwa miguu
lililopo maeneo ya furahisha, jijini Mwanza.
Profesa
Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja huo
kutaimarisha hali ya usafiri wa anga kwa wakazi wa Mwanza na mikoa
mingine na hivyo kukuza shughuli za kibiashara nchini.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wananchi wa Mwanza kutoharibu
miundombinu ya barabara na madaraja ambayo Serikali inatumia gharama
kubwa katika utengenezaji wake.
“Naomba muitunze na kuithamini miundombinu hii kwani Serikali inatumia gharama kubwa katika kutengeneza na kukarabati”, aisema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇