Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, mwenye kofia nyeusi, akiendelea na mazoezi ya Jogging pamoja na vikundi mbalimbali
Vikundi mbalimbali vikiendelea na Jogging
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikabidhiwa Risala na Mwenyekiti wa kikundi cha Newa Life Jogging,Baraka Urio akiwa ameambatana na wanachama wa kikundi hicho,mara baada ya kuisoma na kuelezea changamoto na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya kikundi hicho.Kikundi hicho chenye makazi yake Tabata Mawenzi leo kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza ma vikundi mbalimbali vya mazoezi vilivyoshiriki kwenye hafla fupi ya kutimizwa mwaka mmoja kikundi cha New Life Jogging.
Mjema aliwataka wanaviikundi vya Joggingi, kutoishia tu katika mazoezi bali kutumia vikundi vyao katika kujijenga kiuchumi kwa kubaini fursa mbalimbali na kuzitumia.
Ametaka vikundi kuwa macho na kutoruhusu vikundi vyao kutumiwa na wahuni na wahalifu mbalimbali wakiwemo watumia dawa za kulevya, panya rodi, makaka na madada poa.
Mjema amewataka viongozi wa vikundi hivyo kubaini changamoto na fursa wanazoona kuwa zinaweza kuwasaidia katika kuinua maisha ya wanavikundi wao na wanapobaini fursa au kukumbwa na changamoto wafike mara moja katika Ofisi yake ili kumuona mwenyewe au wasaidizi au maofisa katika ofisi yake.
"Lakini wale waliotaka kuingiza uhalifu,waliotaka kupenyeza madawa ya kulevya ,waliotaka kuingiza siasa,waliotaka kuingiza Panya rodi washindwe na walegee,hatutaki Jogging zetu zichafuke, tunataka Jogging zitumike kuona fursa zilizopo",alisema Mjema.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikabidhiwa jezi na Mwenyekiti wa kikundi cha New Life Jogging,Baraka Urio,pichani kati ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo na wadau wengine wakishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema na viongozi wengine waandamizi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha New Life Jogging,ambacho leo kinasherehekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇