Dr. Stephen Nindi(katikati) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe walipotembelea eneo la upimaji.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe akipongeza hatua ya upimaji wa ardhi na kuahidi kuendelea kutembelea kuona maendeleo
Bw. Ally Amri(kushoto) ambaye ni Land Surveyor akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe namna zoezi la upimaji linavyofanyika
Christian Thomas(aliyevaa shati la blue) ambaye ni mwenyekiti wa kijiji akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe namna zoezi la upimaji wa Ardhi lilivyo wasaidia
Viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wakiwa katika eneo la moja ya kijiji kuona jinsi shughuli za upimaji zinavyokwenda
Hiki ni kifaa kiitwacho Real Time Kinematic (RTK) ni moja ya kifaa cha kisasa kinachotumika katika upimaji wa ardhi.
Bw. Charles Charokiwa Msumari(katikati) Afisa Mifugo Msaidizi Mkuu wa Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe alipotembelea kituo chao ambacho wanakitumia kukusanyia taarifa mbalimbali na shughuli zao
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiendelea kufuatilia kwa makini maelezo
Mtaalam wa GIS Theonest Mlolewe akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe (hayupo pichani) namna wanavyofanya kazi.
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa
MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Stephen Kebwe amesema kazi ya upangaji wa matumizi bora ya ardhi kwa
kiasi kikubwa itapunguza na kuondoa migogoro mbalimbali ya ardhi
inayotokea katika kijiji kwa kijiji,kata kwa kata au kitongoji kwa
kitongoji na kusisitiza kuwa Serikali
haitashindwa kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakaekwamisha kazi
ya upimaji wa ardhi yenye lengo la upangaji wa matumizi bora ya ardhi.
Akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha
Dihombo,Dkt.Kebwe alisema kazi hiyo itasimamiwa kikamilifu na kamati husika za
ulinzi na usalama kutoka Wilayani,Kata hadi Mkoa kuhakikisha inafanikiwa. Alisema
kazi hiyo inayofanywa ya upimaji wa ardhi itakuwa ndio muarobaini wa kuondoa
migogoro inayojitokeza mara kwa mara ikiwemo ya Wakulima na Wafugaji katika
mkoa huo.
Alisema kwa sasa wapimaji wa ardhi wanatumia vipimo vya kisasa zaidi ambavyo
kwa kiasi kikubwa vipimo hivyo vitaweza kupima ardhi kwa kipindi kifupi na kila
mtu kumiliki kipande cha eneo lake.
"Nakumbuka wakati wa kampeni mwaka jana,Rais Dkt.John Magufuli alihaidi
wazi kuwa kipindi cha miaka 10 kutakuwa na upimaji katika maeneo yote ya nchi
kwa utaratibu wa mpango mzuri na wa kisasa,kwa miaka mitano hii vijiji
takribani 7500 vitapimwa kwa kupangwa kila halmashauri 25 ambapo kwa kila
mwaka vitapimwa vijiji 1500,"alisema. Alisema kuwa zoezi la upimaji
linaloendelea hivi sasa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM)kwa wananchi katika kuondoa migogoro inayojitokeza.
"Kazi hii ya upimaji wa maeneo katika kuhakikisha kunampango bora wa
matumizi ya ardhi ni mpango wa nchi,ambapo serikali imechangua Mkoa wa Morogoro
kuwa wa Mfano katika upimaji wa ardhi ambapo utahusisha nchi
nzima,"alisema Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya
Mipango na Matumizi ya Ardhi(NLUPC),Dkt.Stephen Nindi alisema ofisi yake
inafanya kazi na wadau mbalimbali wa masuala ya ardhi zikiwepo wizara pamoja na
mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali ikiwemo Shirika la Kimataifa la
Care,Shirika la Oxfam,Chama cha Wafugaji Tanzania,Chuo kikuu cha Ardhi pamoja
na Tamisemi.
Dkt.Nindi alisema kwa sasa kazi ya ya upimaji inafanywa na vifaa maalum vya
kisasa vijulikanavyo kwa jina la Real Time Kinematic ambavyo vinafanya kazi kwa
urahisi zaidi,licha ya vifaa hivyo kwa sasa vipo viwili nanvyakukodisha. "Tunahitaji
kuwa na vifaa hivi walau vitano ambavyo vitatuwezesha kupima kwa wakati na
kukaimilisha zoezi hili kwa haraka na kifaa kimoja kinagharimu kiasi cha
sh.milioni 80,"alisema Dkt Nindi
Naye Mratibu wa Programu ya Ufugaji Asili kutoka Shirika la Kimataifa la
Care,Marcely Madubi alisema suala la ardhi ni moja ya masuala muhimu
yanayozingatiwa na shirika lao katika mikakati yao ya kimataifa. Alisema wadau
mbalimbali nchini wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuchangia suala hili la
kuhakikisha upimaji wa ardhi unafanikiwa hususani katika kuchangia ununuzi wa
vifaa vya teknolojia mpya ya upimaji(Real Time Kinematic)ili kuwezesha upimaji
wa ardhi kwenda kwa haraka zaidi na kupunguza migogoro inayoendelea
kujitokeza.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇