RAIS JOHN POMBE MAGUFULI |
Uongozi ni hali ya muhusika mmoja kuwa na dhamana, madaraka na uwezo wa kuwaongoza wengine. Ili uwepo uongozi lazima awepo kiongozi na wanao ongozwa. Kiongozi anaweza kuwa rais, waziri, mbunge, mtemi, mfalme, mkurugenzi, chifu, na hata muwakilishi wa wengine kama vile mwenyekiti au mjumbe wote ni viongozi.Tangu Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani, mambo mengi yamebadilika kuanzia utendaji kazi wa viongozi mpaka wananchi wa kawaida.
Kutokana na mabadiliko hayo, nimeamua kuandika makala kuwafunda viongozi waliopo madarakani kama wajumbe wa serikali za mitaa, wenyeviti, madiwani, wabunge na mawaziri ni sifa zipi wawe nazo na kuwajuza Watanzania kwa ujumla mabadiliko aliyoyaleta Rais John Pombe Magufuli na jinsi ya kwenda sambamba na kasi yake.
SIFA KUU ZA KIONGOZI
Kiongozi yoyote duniani ili awe bora ni lazima awe na sifa kadhaa ambazo zitasababisha kukubalika na jamii anayoiongoza na kukabiliana na changamotop mbalimbali, sifa zipo nyingi ila kwenye makala hii nitazitaja baadhi;-
Mosi, akili timamu (ufahamu), kiongozi ni lazima awe mjuzi dhidi ya kundi kubwa analoliongoza katika nyanja tofauti kama vile mazingira, tamaduni, mila na desturi na matatizo ya anao waongoza.
Pili, maadili mema ambayo hujumuisha vitu vingi ikiwemo tabia njema, ucha Mungu na uadilifu, bila kuwa na maadili mema huwezi kuwa muadilifu hivyo maaadili ni sifa ya msingi kwa kiongozi kwani itasababisha kukubalika na jamii anayoiongoza.
Tatu, uaminifu, ili kufikia malengo kwa jamii yoyote au taasisi lazima uwepo kiongozi mwaminifu. Shabaha ama malengo hayata timia ikiwa kiongozi si mwanifu kwa watu anao waongoza. Uamini ni pamoja na kufanya yale aliyoagizwa bila upendeleo wala kuangalia maslahi ya kundi lolote ispo kuwa maslahi ya anao waongoza.
Tanzania kwa awamu zote zilizopita imekuwa ikipata viongozi wenye sifa ya kuwa viongozi ndio maana jamii ikawakubali na kuwapa ridhaa ya kuwa viongozi. Katika kuiongoza jamii ya watu wapatao takribani watu milioni 44.9 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2012 changamoto ni lazima.
Zimejitokeza changamoto nyingi kubwa na ndogo katika awamu nne zilizopita. Kila awamu na changamoto zake, kila awamu na jitihada zake katika kuikwamua nchi dhidi ya changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hali kisiasa iwe shwari kuilingania nchi swala la amani, upatikanaji wa huduma za afya na mahitaji muhimu pia swala la nchi kuingia uchumi wa kati.
Tanzania imekuwa mpya, mfumo wa maisha umebadilika, serikali ya awamu ya tano imebadilisha mfumo wa maisha kuanzia ngazi ya familia, serikali za mitaa mpaka serikali kuu imekuwa tofauti na awamu nne zilizopita.
Pia tangu Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani, kuna mambo mengi ambayo yalikuwa yanafanywa kwa mazoea, kwa namna moja ama nyingine yameisha, mambo yako mengi baadhi yake ni;-
ULIPAJI KODI.
Serikali ya awamu ya Tano ni serikali tofauti kidogo na awamu zingine zilizopita, si kwamba awamu zingine wananchi na mashirika binafsi hawakulipa kodi hapana, serikali ya awamu ya Tano inafuatilia kwa kiasi kikubwa swala la kodi.
Shirika la fedha la kimataifa (IMF) limelipoti kuwa Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016, kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara.
Haya ni matunda ya ukusanyaji wa kodi na utumiaji sahihi wa mapato yanayokusanywa na mamlaka ya mapato TRA, hivyo tumehama katika kutegemea wahisani na nchi inaanza kuendeshwa kwa kodi za wananchi.
UWAJIBIKAJI.
Tanzania imekuwa nchi ya uwajibikaji kwa kila mwananchi, kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa kwa ujumla kila mmoja anawajibika katika nafasi yake ni kweli pesa imekuwa ngumu kuipata kwa asiyewajibika kufanya kazi na wanaojipatia pesa kwa njia za ujanja ujanja ila kwa waliojikita katika shughuli za halali wanaona hali ya kawaida.
Serikali ya Awamu ya Tano imebaini mradi wa wafanya kazi hewa serikalini, ubadhirifu wa fedha za umma katika sekta mbali mbali na mashirika yenye umri mrefu katika utendaji bila kulipa kodi.
UCHAPAKAZI.
Serikali ya awamu ya Tano ni ya uchapakazi, mwanachi asiye na sifa ya uchapakazi lazima ataona ugumu wa maisha na watumishi wa serikali wasio na sifa hii wana wakati mgumu na hata mashirika binafsi kwani kigezo cha kodi kinamuwajibisha kila mmoja kuivaa sifa ya uchapakazi.
Rekodi ya muheshimiwa, Rais John Pombe Magufuli tangu akiwa Waziri ni uchapakasi na kasi aliyoanza nayo ni uchapakazi, kitendo hicho kinahamasisha viongozi na wananchi kwa ujumla kuwa wachapakazi, hivyo tutaipata Tanzania mpya ya uchapakazi katika shughuli za ujenzi wa Taifa.
MAADILI
.
Tanzania ya awamu ya Tano ni Tanzania inayomulika ipasavyo swala la maadili kwa jamii. Katika mitandao ya kijamii kipindi cha nyuma wanajamii walikuwa wakitumia vyombo hivyo bila kuhofia mkono wa serikali. Awamu ya Tano imeshawatia nguvuni wavunja amani mitandano kwa kutoa maneno ya uchochezi, taarifa za uzushi na matusi.
Pia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli alitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa, Charles Kitwanga, mei ,20 mwaka huu kwa kosa la kutokuwa na maadili mema kwa kitendo chake cha kushiriki shughuli za Bunge akiwa amelewa.
KUJITEGEMEA.
Serikali ya Awamu ya Tano iliwashtua wananchi baada ya Muheshimiwa Rais kukataa baadhi ya misaada kutoka nje, Tanzania mpya inamjengea mtanzania hali ya kujitegemea kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa kwaujumla.
Nchi inayotegemea misaada ya kutoka nchi zilizoendelea, itaendelea kunyonywa kiuchumi na kila siku itakuwa nyuma kiuchumi. Hakuna Taifa lililokuwa kiuchumi kwa kutegemea misaada mpaka mwisho, mapato ya nchi ndio yanakuza uchumi wa nchi.
MUANDAAJI. NASSIR BAKARI
OFISI NDOGO ZA CCM
LUMUMBA
PHONE:0713 311 300
EMAIL: nassiribakari@gmail.com
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇