MOHAMMED GOMBELA |
WAJUMBE wawili wa nyumba kumi katika mtaa wa Msufini, Chamazi, Dar es Salaam, Mohammed Gombela na Biti Mzee, wamejiuzuru nyadhifa zao, kutokana na madai ya kukataa kuchonganishwa na wananchi kuhusu suala la ulinzi shirikishi.
Akizungumza jana, Gombela ambaye ni mjumbe wa shina namba 41, alisema wameamua kujiuzuru kutokana na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wao Salum Msoma, kuwataka wale nae njama za kuandika majina ya wananchi ambao hawashiriki ulinzi huo kisha wayapeleke Serikali ya mtaa, ili wakamatwe siku ya ijumaa na kuachiwa huru Jumatatu baada ya kukaa mahabusu Jumamosi na Jumapili ili kuwakomoa.
“Mimi kama mjumbe wa nyumba kumi, shina namba 21, nimeamua kujiuzuru nyazifa yangu na muda si mrefu nitaipeleka rasmi barua ya kujizuru, mwenzangu Biti Mzee amekwishapeleka, kiukweli Mwenyekiti hakutenda haki, kwa sababu tulimwita kwenye kikao ambacho saa kumi kujadili na wananchi kuhusu suala hilo la ulinzi, akasema anakuja, lakin ilipofika saa nane, akatoa taarifa kuwa hatofika, anaenda msibani,” alisema Gombela.
“Kutokana na kwamba alitoa taarifa ya kutofika huku wananchi wengi wakiwa wamefika kwenye kikao, hatukuweza kukiahirisha, kikao kilifanyika na ilipofika muda wa maswali baadhi ya wananchi wakataka kupata ufafanuzi wa mambo mengi ikiwemo wakiumia wakati wa ulinzi nani anawajibika, lakini wakuyajibu kwa kuwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa hakuwepo ikawa hakuna wa kutoa ufafanuzi wa masuala hayo” alisema Gombela.
Alisema, baada ya kumaliza kikao na wananchi kutopata majibu ya maswali yao, walitarajia Mwenyekiti ataitisha kikao kingine, lakini hakuitisha, baadae wa kaletewa barua ikiwataka wawaambie wananchi walinde na asiyelinda, wamwandike jina na kulipeleka kwa Mwenyekiti huyo ili apelekwe mahabusu.
" Je kutokana na maelekezo hayo, hapo siyo kutafutiana lawama? Kwa sababu hizo mimi na mjumbe mwenzangu, tumeamua kujiuzuru na kuwapisha wananchi wengine wachaguliwe, ila sisi hatutaki lawama, maana leo mtu unampeleka polisi kesho akitoka atakuonaje?,” alisema Gombela.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇