GAVANA WA BENKI KUU NDULU |
Na Abushehe Nondo na Lilian Lundo,
Maelezo.
Kasi ya ukuaji wa pato la Taifa kwa nusu ya kwanza ya mwaka yaani Januari
mpaka Juni 2016 imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia
5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Benno
Ndulu alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu , hali ya ukuaji wa
uchumi wa Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha ambapo katika robo ya pili ya mwaka 2016
ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa asilimia 5.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015.
Ndulu alisema kuwa shughuli za kiuchumi
ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka
2016 kuwa ni pamoja naUsafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 30.6,
uchimbaji wa madini asilimia 20.5, Mawasiliano na Habari asilimia 12.6 na Sekta
ya fedha na Bima asilimia 12.5.
Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na
ujifadhi wa mizigo umetokana na kuongezeka kwa usafirishaji wa abiria kwa njia
ya biashara na gesi asili ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo
ya pili ya mwaka 2015 kwa asilimia 9.4.
Akizungumzia hali ya ukuaji wa uchumi
kwa nusu ya mwaka 2016 Ndulu alisema kuwa katika nusu ya kwanza ya Januari hadi Juni mwaka 2016 kasi ya ukuaji
wa pato la Taifa umeendelea kukua kwa kasi kutokana na baadhi ya sekta
kuonekana kukua zaidi ikiwemo Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo asilimia 17.4
Sekta nyingine ambayo imekua kwa kasi
kwa kipindi hicho ni pamoja na sekta ya Uchimbaji wa Madini na Gesi asilimia
13.7, Mawasiliano asilimia 13.0 na sekta ya fedha na Bima asilimia 13.0.
Akifafanua michango ya shughuli
mbalimbali zilizochangia ukuaji wa
kiuchumi katika nusu ya kwanza ya
Mwaka huo alizitaja kuwa ni pamoja na Uchukuzi na Uhifadhi Mizigo asilimia 16.0, Ujenzi asilimia 10.7,
na Sekta ya Kilimo ambayo inaonekana kukua kwa asilimia 10.3 katika nusu ya
kwanza ya mwaka 2016.
Aidha alisema kuwa kwa kuangalia hali ya
ukuaji wa pato la Taifa kwa nusu ya kwanza ya mwaka pamoja na viashiria
mbalimbali vya uchumi ni mategemeo yao kwamba pato la Taifa kukua kwa asilimia
7.2 kwa mwaka 2016 litafikiwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇