Na
Mwandishi Maalum, New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon, ameitaka
Tanzania kuendelea na kazi nzuri
ya usuluhishi wa migogoro
katika baadhi ya nchi za Maziwa
Makuu.
Ban Ki Moon ametoa wito huo jana ( jumatano) wakati alipokutana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Dk. Augustine Mahiga, ambaye
anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika mkutano wa
71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea hapa Jijini New York, Marekani.
Katika mazungumzo hayo Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema, Tanzania ni
kutovu cha Amani, usalama na demokrasia, na
kutokana na sifa hizo Tanzania,
inapashwa kuendelea na juhudi zake za kuzisaidia nchi zenye migogoro.
Akazitaja nchi hizo kuwa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,
Burundi na Sudani ya Kusini ambayo
ameitaja kuwa ipo katika kipindi kigumu
sana.
“ Ninawashukuru sana viongozi
wa Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri ya utafutaji wa Amani katika nchi zenye matatizo, Sudani ya Kusini ni nchi ambayo inatupa mashaka makubwa. Rais asaidie katika
kurejesha hali ya utulivu.Tanzania
ni nchi kubwa kwa hiyo bado ninaendelea kuitumainia.” akasisitiza Ban Ki Moon.
Vile vile Katibu Mkuu Ban Ki Moon
ametoa pia shukrani wa ushiriki wa Tanzania katika operesheni za ulinzi wa Amani na kazi na
weledi mkubwa unaoonyeshwa na
wanajeshi wa Tanzania.
Akatumia fursa hii kuishukuru
Tanzania na viongozi wake kwa
mchango wao mkubwa uliofanikisha
yeye kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Na akatoa pole
zake kwa serikali na kwa watanzania baada ya kupata taarifa kuhusu tetemeko la ardhi lililosababisha vifo na
uharibifu wa mali.
“Naishukuru sana Tanzania, namshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kiwete na wewe
( Waziri) na viongozi wengine, mlichangia sana kwangu mimi kuwa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa. Ninawashukuru sana sana.
” .
Katibu Mkuu Ban Ki Moon anamaliza kipindi chake cha
uongozi cha miaka kumi
mwishoni wa Mwaka huu.Na
tayari mchakato wa upigaji kura wakumtafuta mrithi wake
unaendelea katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake, akiwasilisha salamau za Rais John Pombe Magufuli, Waziri Mahiga amesema. “ Ninawasilisha salamu za Mhe. Rais,
alipenda sana kuhudhuria mkutano huu wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, kwa bahati mbaya ilimbidi kuahirisha safari yake kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibu
nchini kwetu ”.
Aidha Waziri Mahinga ametumia pia fursa hiyo
kumshukuru na kumpongeza Katibu Mkuu
kwa utekelezaji wa kutukuka wa majukumu yake
katika kipindi cha miaka kumi ya
uongozi wake.
“Kwa niaba ya serikali ya
Tanzania nikupongeza kwa utekeleaji wa majukumu yake. Ulionyesha
ushirikiano wa karibu na Tanzania,
ushirikiano uliokuwezesha kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Naibu
Katibu Mkuu na msaidizi wako wa karibu. Lakini pia uliniteua mimi kuwa
Mjumbe wako Maalum huko Somalia
. Tanzania inashukuru kwa haya na mengine” akasema Mahiga.
Aidha
amemwelezea Katibu Mkuu kama kiongozi ambaye aliifanya Afrika kuwa
kipaumbele chake, lakini pia aliibeba
sana ajenda ya wanawake jambo ambalo
amesema limemjenga sifa kubwa.
Akizungumzia kuhusu Tanzania kuendelea
na juhudi za usuluhishi wa migogoro. Waziri amemhakikisha Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa kwamba, Tanzania na viongozi wake wataendelea na kujukumu
hilo.
“Ni kuhakikishie kwamba Serikali
yangu itendelea na jukumu hili la usuluhisi. Na kwa upande wa Burundi Tanzania,
inaushukuru Umoja wa Mataifa, kwa
kutambua na kuamini kwamba Jumuiya ya
Afrika Mashariki inaweza kuushughulikia mgogoro huu. Tanzania ambayo imekabidhiwa jukumu la
uwezeshaji wa mazungumzo ya Amani inataka kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa
Mataifa hivyo misaada ya hali na mali kutoka Idara za
Umoja wa Matifa ni jambo muhimu”.Amesisitiza Waziri Mahiga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇