LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 29, 2016

SERIKALI YAFUNGIA VITUO VYA REDIO VYA MAGIC FM NA REDIO 5 YA ARUSHA KUANZIA LEO

WAZIRI NAPE
Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Serikali imevifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Dadio vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam, kwa kudaiwa kukiuka maadili na kanuni za utangazaji.

Kufungiwa kwa vituo hivyo kumetangazwa leo jijini Dar es Salaam, na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akisema kwamba vituo hivyo kwa nyakati tofauti vilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi.

“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.

Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.

Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani na ushirikiano nchini na sio vinginevyo.

Hivi karibuni, Nape alitahadharisha kuwa vyombo vya habari vitakavyoripoti taarifa ambazo ni za uchochezi vitakumbwa na rungu la kuhusika kwa uchochezi pia.

VIDEO : WAZIRI NAPE AKITANGAZA KUFUNGIWA KWA VITUO HIVYO

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages