LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2016

SERIKALI SIMIYU YAAMUA ASILIMIA MBILI YA USHURU WA PAMBA IJENGE MADARASA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka (Katikati) akizungumza na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe. Festo S. Kiswaga  
  Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, mstari wa kwanza kutoka kushoto, Mhe. Benson Kilangi (Itilima), Joseph Chilongani (Meatu), Seif Shekalaghe, Tano Mwera (Busega) na mstari wa pili, kutoka kushoto, Mhe. Stanslaus Nyongo(Mbunge Maswa Mashariki), Mhe. Mashimba Ndaki (Mbunge Maswa Magharibi).
  Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (kulia) ili azungumze na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Viongozi na baadhi Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Maswa, Mhe. Dila Mayeka akitoa mchango wake wa mawazo katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, kilichofanyika Mjini Bariadi


Na Stella Kalinga
Serikali Mkoani Simiyu imesema  asilimia mbili ya ushuru wa zao la pamba inayopatikana katika Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu ielekezwe katika ujenzi wa Miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari,hususani vyumba vya madarasa.
Uamuzi huo umefikiwa kufuatia majadiliano ya pamoja kati ya Uongozi wa Mkoa na Halmashauri zote katika kikao  kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka akiwa na Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wilaya na Wajumbe wa Kamati za Fedha za Halmashauri ili kujadili mstakabali wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika mkoa huo.
Mtaka amewaelekeza Wakurugezi wote wakafanye uhakiki na kuainisha takwimu sahihi  za mahitaji ya vyumba vya madarasa ili kupata uhakika wa vyumba vinavyohitajika katika mkoa mzima na kupanga mkakati wa namna vyumba hivyo vitakavyojengwa ikiwa ni pamoja na teknolojia itakayotumika katika kufyatua matofali  pamoja na gharama zake na kuwasilisha taarifa katika Ofisi yake tarehe 9 Agosti, 2016, ambapo baada ya kupata taarifa hiyo na kujiridhisha zoezi la ufyatuaji matofali kimkoa litazinduliwa rasmi Wilayani Maswa tarehe itakayopangwa na mkoa.
“ Sina uhakika sana na takwimu hizi, niwaagize tena Wakurugenzi wote mkafanye mapitio upya na uhakiki wa kina katika maeneo yenu juu ya idadi ya vyumba vya madarasa vinavyohitajika kwa Elimu ya Msingi na Sekondari. Mkae na wataalam wenu wa ujenzi mfanye tathmini ya namna mtakavyojenga kama mtatumia matofali ya kuchoma, matofali ya block au matofali yakufungamana (interlocking blocks) yanayofyatuliwa na vijana waliopewa mafunzo na Shirika la Nyumba la Taifa,ambao wako katika kila halmashauri pamoja na gharama zitakazotumika”, alisema Mtaka.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amewataka Wakurugenzi kufanya utaratibu wa kubadilisha matumizi ya fedha haraka  pale inapobidi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu kufanikisha zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwatengenezea wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunzia na kuwezesha madawati yaliyotengenezwa ambayo hayana mahali pa kuwekwa yasihar

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages