WAZIRI NAPE |
Serikali inatarajia kutatangaza zabuni kwa ajili ya kupata kampuni itayojenga kijiji cha michezo changamani kilichopo Temeke Jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati akipokea uwanja wa Uhuru kutoka kwa kampuni ya CBG baada ya kufanyiwa matengenezo.
Mhe. Nape Moses Nnauye amesema kuwa azma ya kujenga kijiji cha changamani ni ya muda mrefu na kuna mchakato wa kutengeneza ubia kati ya Serikali na wadau wengine wa michezo ili kutekeleza mradi huo.
“ Tutatangaza zabuni kwa makampuni ili waweze kutuma maombi yao kwa ajili ya kutekeleza mradi huu na tutapitia kwa kina na umakini maombi yote ili kupata mtu sahihi” alisema Mhe. Nape.
Mhe. Nape Moses Nnauye ameongeza kuwa Serikali tayari imeshaandaa eneo na ramani kwa ajili ya ujenzi na hivyo kuwapa nafasi wadau watakaopenda kujenga mradi huo.
Amesisitiza kuwa mchakato huo sio wa siku moja kwa kuwa kuna taratibu za kisheria zinahitajika kufuatwa ili kutekeleza mradi huo katika viwango vya kimataifa.
Eneo changamani ni eneo la kwa ajili ya ujenzi viwanja vingi vya michezo vitakavyotumika katika kukuza na kuinua vipaji vya michezo nchini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇