Na Nassir Bakari 0713 311 300
Ile hali ya sintofahamu iliyoanza kujitokeza tangu tarehe
21/08/2016 kwenye ukumbi wa Blue Pearl , Ubungo Plaza, Dar es Salaam kwenye
mkutano mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), imeendelea baada ya Naibu Katibu Mkuu
wa chama hicho ndugu Nassor Ahmed Mazrui, kuwaita wazee wa chama hicho ‘waongo’
baada ya wazee hao kufanya mkutano na kusema Maalim Seif anakigawa chama.
Kauli hiyo imekuja siku moja, baada ya wazee wa chama hicho wa
mkoa wa Dar es Salaam, kuitisha kikao na waandishi wa habari kilichoongozwa
na Katibu wa wazee wa chama hicho mkoa
wa Dar es Salaam, Abdul Rajabu Magomba na kusema kuwa kuna mkakati wa makusudi
unaofanywa na katibu mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad wa kukiua chama hicho kwa
upande wa Tanganyika.
Akijibu shutuma hizo Naibu katibu mkuu wa chama hicho, ndugu
Nassor Ahmed Mazrui alisema yote yaliyozungumzwa na wazee hao, sio ya kweli na hayana mashiko.
“Yote hayo ni uongo mtupu, Chama kikiwa cha upande mmoja
kinafutwa na Msajili leo Maalim awe mjinga kiasi gani hata agawe Chama.”
Pia, katibu mkuu huyo aligusia swala la aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama hicho, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, kurejea kwenye nafasi yake ya
uenyekiti wa chama hicho na kusema hata iweje chama cha wananchi(CUF),
hakitoweza kumruhusu kurudi tena kwenye nafasi hiyo.
“Sasa utamrejesha mtu aliyejiuzulu ndugu yangu, mimi
ningemshauri asubiri hadi mwaka 2018.”
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇