Marcelin Ndimbwa |
Akizungumza leo, Ndimbwa amesema pamoja na ekari 45 walizopewa,
pia watapewa bure mbegu, na baada ya kupanda itawachukua siku 85 mavuno kuwa
tayari ambapo mujibu wa msimamizi wa mradi huo Ofisa Kilimo, Mhandisi, Maimuna
Makutika ekari moja lina uwezo wa kutoa magunia 40 hadi 50.
Fisa kilimo huyo ameongeza kwamba gharama ya kuhudumia ekari moja
hadi kufikia hatua ya mavuno haizidi 600,000, huku gunia moja kwa wastani wa
bei, mwezi Desemba hadi Janauari huzwa kwa sh 80,000 hadi 120,000, hivyo kwa
wastani ekari 45 zitatoa kiasi cha sh 180,000,000.
Mkurugenzi Ndimbwa amesema kupitia uwekezaji huo vijana watakua
wamepata ajira ya kudumu na pia watakua wamejikwamua kiuchumi kama
watafanya bidii na kuyatunza mashamba hayo inavyostahili.
Pia Mkurugenzi amesema kupitia mradi huu wa kilimo uchumi wa watu
wa Malinyi utakua pamoja na kuhamasisha jamii inayozunguka wilaya hiyo
kujiajiri kwa kuwekeza katika Kilimo ili kujikwamua kutoka katika wimbi la
umasikini na kuongza kuwa tayari vikundi vya vijana wilayani hapo vimehamasika
baada ya kuona mwitikio wa wasomi kuwekeza kwenye kilimo ambapo hadi sasa
vijana wenyeji walioitikia ni zaidi ya 150, vikundi 30 na ekari zaidi ya 200
zishalimwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇