LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 21, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEWATAKA WATENDAJI WA IDARA YA MAZINGIRA KATIKA OFISI YAKE WAJIPANGE VIZURI KWA AJILI YA KUFANYA TATHMINI YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA MJINI DODOMA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha kazi kilichodumu kwa siku mbili ambao alipokea na kujadili masuala mbali mbali yanayohusu mazingira, kulia ni Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
 Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha Idara ya Mazingira kilichoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira na Wakuu wa Vitengo, waliokaa pamoja na Makamu wa Rais kushoto ni  Waziri Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais  Ndugu Mbaraka Abdulwakil.
                                                             ...........................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa Idara ya Mazingira katika ofisi yake wajipange vizuri kwa ajili ya kufanya tathmini ya athari za kimazingira mjini Dodoma wakati serikali ikijiandaa kuhamia kwenye mji huo.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 21-Aug-16 alipokuwa akifunga mkutano wa kazi wa siku mbili na watendaji wa Idara ya Mazingira ambapo walijadili namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea kote nchini.

Ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuuweka mji wa Dodoma salama kimazingira ikiwemo ubora wa miundombinu za maji taka.


Makamu wa Rais amesema kutokana na idadi kubwa ya watu hasa watumishi ambao watahamia Dodoma bila miundombinu imara hali ya uchafuzi wa mazingira itakuwa si nzuri hivyo ni muhimu kwa watendaji hao kuweka mipango na mikakati madhubuti ya kuhakikisha mji wa Dodoma hautaathirika kimazingira.

Kuhusu utendaji kazi wa watumishi wa ofisi yake amewataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa uwazi katika matumizi ya fedha za miradi na hasa  inayohusika na uhifadhi wa mazingira jambo ambalo litaondoa manung'uniko miongoni mwa watumishi na wananchi kwa ujumla.


Amesema ushirikiano huo miongoni mwa watumishi utasaidia kwa kiasi kikubwa ufanisi katika kazi za kila siku ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Makamu wa Rais amesema ataendelea na utaratibu wa kukutana na watumishi kila baada ya miezi 4 katika ngazi ya viongozi kama hatua ya kujitathmini katika mipango ya kazi waliyojiwekea.
 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages