Na Mwandishi Maalum
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kwa namna moja ama nyingine utekelezaji wa lengo namba Nne ya Maendeleo
Endelevu kuhusu Elimu la
Maendeleo Endelevu (SDG4) kwa kutoa elimu
bure kuanzia shule ya msingi hadi
sekondari ikiwa ni pamoja na kuifanya
jumuishi kwa makundi yote ya
jamii wakiwamo walemavu wa aina
mbalimbali.
Hayo yameelezwa
na Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Matifa, Balozi
Tuvako Manongi wakati wa majadiliano kuhusu utekelezaji wa
lengo namba Nne ambalo ni kati ya Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu, maarufu kama agenda 2030 yaliyopitishwa mwezi
septemba mwaka jana na viongozi
wakuu wa nchi na serikali.
Balozi Manongi
alikuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika
majadiliano hayo, ambayo yalimhusisha pia Waziri Mkuu wa Norway, Mhe.
Erna Solberg na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bakova na yaliandaliwa kwa ushirikiano wa UNESCO
na UNICEF kama sehemu ya Mkutano wa Kilele wa Kisiasa wa Baraza
la Uchumi la Umoja wa Mataifa ( ECOSOC) unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa.
SGD4
pamoja na mambo mengine inatilia
mkazo na kutoa kipaumbele cha pekee
katika utoaji na upatikanaji wa elimu
ambayo ni jumuishi, yenye ubora na
inayowafikia makundi yote ya jamii, hususani watoto, wanawake na walemavu.
Akielezea namna Tanzania ilivyojipanga katika utekelezaji wa SDG4 kwa sasa
na kwa baaday,Balozi Manongi amesema
Tanzania imejipaga vema kisera, kisheria na kimkakati katika kuhakikisha kwamba kila mtanzania bila kujali ni wa kundi gani anapata fursa ya elimu na si elimu tu bali elimu yenye ubora wa hali ya juu na inayokidhi mahitaji na mazingira ya sasa.
Pamoja na
kuainisha sera na sheria mbalimbali ambazo serikali inazitekeleza katika eneo
hilo la elimu, Balozi Manongi anasema,
kuwa na sera nzuri, sheria nzuri na mikakati mizuri hakuwezi kuwa kigezo
pekee cha kufanikisha utekelezaji wa
SDG4.
“ Kwa
Tanzania tatizo siyo sera, sheria au
mipango na mikakati, tatizo ni raslimali fedha ya kutosha ( bajeti) itakayowezsha
utekelezaji wa SDG4 na malengo mengine
kwa ukamilifu unaotakiwa”. Anasema
Balozi
Kutokana na changamato
hiyo ya ufinyu wa raslimali
fedha, Mwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
anasisitiza haja na umuhimu wa ushirikiano wa karibu baina ya
Serikali Kuu, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuhakikisha
kwamba hakuna yeyote atakaye achwa
nyuma.
Akizungumzia zaidi
utekelezaji wa SGD4 achia
mbali utoaji wa elimu bure kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari,
na kuhakikisha elimu inawafikia wote,
Balozi Manongi amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba hivi karibuni Serikali imetangaza kutenga kiasi cha fedha
kwaajili ya kuwasomesha watu wenye matatizo ya ualibino.
“pamoja na changamoto mbalimbali serikali yangu inajitahidi sana kuyafikia
makundi mbalimbali ya jamii, wawe ni
watoto wa kike, watoto wanaoishi katika
mazingira magumu, ama jamii za wafugaji
na wawindaji lakini pia imekwenda mbali
zaidi katika kuhakikisha kwamba jamii
yenye mahitaji maalum nayo inafikiwa”
akasisitiza Balozi Manongi.
Akizungumzia
zaidi kuhusu uamuzi wa Serikali ya awamu ya Tano wa kuifanya elimu ya msingi hadi Sekondari kuwa bure. Balozi amewaeleza wajumbe wa majadiliano hayo
kwamba, maana ya uamuzi huo ni kuwa mtoto wa kitanzania atafaidika na elimu ya bure kwa miaka kumi na moja. Na vile vile
Tanzania inakuwa sehemu ya
utekelezaji wa baadhi ya kipengele cha SDG4 kinachopendekeza utoaji wa
elimu bure ili iwafikia watu wengi
zaidi.
Washiriki
wengine katika majadiliano hayo walikuwa
ni Mwakilishi wa Kudumu ya Jamhuri ya Korea Balozi Oh Joon ambaye pia
ni Rais wa ECOSOC, Waziri wa Elimu
kutoka Bolivia Bw. Bw. Roberto Iván Aguilar Gómez, Bw. Guy Ryder, Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Kazi Duniani (ILO) Mwakilishi wa Kudumu wa
Ufalme wa Morroco katika Umoja wa Mataifa, Balozi Omar Hilale, Bi. Alice
Albright kutoka Global Partnership for
Education (GPE),Bi Silvia Montoya, kutoka Tasisi ya Takwimu ya UNESCO na Bi. Josephine Bourne kutoka UNCEF.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇