Jana
tarehe 27/7/2016 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walitoa kauli kwa
Waandishi wa Habari kupitia Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Ndugu Freeman Mbowe
(Mb). Tamko hilo kama ilivyo kawaida ya CHADEMA lilijaa uongo mwingi na ghiliba
nyingi za kibabaishaji na kuthibitisha ukweli kuwa kwa hakika kutokana na kasi
ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dr. John Pombe Magufuli wapinzani nchi
hii wamekosa ajenda na hivyo njia peke yake wanayoona inafaa ili waendelee
kufanya utapeli ni kutunga uongo, kujiaminisha katika uongo huo na kuusambaza
uongo huo ili kujaribu kupata wafuasi.
Katika
uongo na uzushi huo walioutangaza jana, CHADEMA wanasema wameamua kufanya
mikutano na maandamano nchi nzima kwa tarehe waliyoitaja na maandamano hayo
yatafanyika chini ya operesheni waliyoiita UKUTA. Kimsingi hoja walizozitumia
kufikia uamuzi wao bila kuzirudia zimejaa upotoshaji na uongo uliokithiri. Kwa
mfano wanadai Serikali imezuia mikutano yote ya vyama vya siasa, huku wakijua
kuwa ni uongo kwani Serikali haijazuia mikutano kwenye majimbo yao, Wabunge
wako huru kufanya shughuli zao kwenye majimbo yao, na tumeona Wabunge wakifanya
shughuli zao majimboni bila shida wakiwemo hao wa vyama vya upinzani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇