RAIS DK. MAGUFULI |
Na Daudi Manongi, MAELEZO.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli amewaagiza
makatibu wakuu wote wa wizara kutumia mashine za kietroniki (EFD) katika kukusanya
mapato serikalini.
Rais
Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa Halmashauri, Wilaya, Majiji
na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu
kwa viongozi hao wa umma.
“Vyombo
vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu
maafisa wa serikali hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende
hivyo”Alisema Rais Magufuli.
Aidha
amewataka wakurugenzi wote kuchukua
mashine hizi na kwenda nazo katika maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika
ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmshauri zao.
Pia
amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi wa chini
zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji wa chini yao
wasioendana na kasi ya awamu ya tano
basi watumie madaraka yao kuwaweka sawa.
Rais
magufuli pia amewaagiza wakurugenzi hao kusimamia ilani ya uchaguzi ya chama
cha mapinduzi kwakuwa
waliahidi kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi
waishi vizuri kwa amani ndani ya nchi yao
na kuongezea kuwa viongozi wa juu wana imani kubwa sana nao ndio maana hata
wakachaguliwa kutoka katika watanzania hawa milioni 50.
Aidha
Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa viwanda vidogo
vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya
kuwa na viwanda.
Mbali
na hayo pia amewataka wakurugenzi hao kubadilika kifikra na kuachana na
kuongoza kwa historia kwani wananchi wa sasa wamebadilika na hivyo wafanye kazi
kwa bidii ili kuwatimizia wananchi yale wanayotaka na hivyo nchi itasonga
mbele.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇