Na Bashir Nkoromo
Rais DK. John Magufuli ameahidi kwamba Serikali yake itaitengeneza barabara kutoka Ubungo Kibangu hadi Riverside itakayoungana na Barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa leo na Ikulu, imesema Rais ametoa ahadi hiyo ameitoa kwa waumini wa Kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) lililopo Ubungo Kibangu
Jijini Dar es Salaam alipotembelea Kanisa hilo leo Juni 5, 2016.
Imesema, Rais
Magufuli ambaye amezungumza katika ibada ya asubuhi ya Kanisa hilo amesema amepita katika barabara hiyo ambayo imekuwa
ikitumiwa na waumini hao na wananchi wengine wa eneo la Ubungo
Kibangu kwa lengo la kujionea hali halisi.
Aidha,
Rais Magufuli amempongeza Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Antony Lusekelo
maarufu kwa jina la Mzee wa Upako kwa
huduma ya maombezi anayoitoa kwa waumini wake na watazamaji wanaofuatilia
vipindi vyake vya Mahubiri kupitia Luninga.
“Mimi
ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa
yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, kwa hiyo
nataka kukuthibitishia ninakupenda sana.
“Ndio
maana kuna siku moja, ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi
nitafute mbinu za namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi, nikamtuma
meneja wa barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu
changamoto zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu, nataka
kukuthibitishia kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo”
Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na waumini.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) amemshukuru Rais Magufuli
kwa kulitembelea kanisa hilo, na amemuombea heri katika uongozi wake ili aweze
kufanikisha azma ya kuliletea taifa maendeleo ikiwemo mpango wa kuanzisha
viwanda.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇