Na Mwandishi Maalum, New York
Viongozi Wakuu wa Polisi kutoka
nchi mia moja ambazo
zinachangia polisi wao kuhudumu katika ulinzi wa amani
na usalama kupitia Umoja wa Mataifa,
wamekamilisha mkutano wao wa siku
moja uliofanyika jana Ijumaa hapa Makao
Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Huu ni mkutano kwa kwanza wa aina yake kuwahi
kufanyika, ambapo wakuu wa Polisi ( IGPs) wamekutana kwa wingi na kwa
wakati mmoja tangu shughuli za
Kipolisi zilipoingizwa
katika Operesheni za Ulinzi wa Amani
kupitia mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.
Katika mkutano huu na ambao washiriki
walijadiliana, kubadilishana uzoefu, na namna ya kukabiliana na changamoto
mbalimbali za kubadilishana za ulinzi
na usalama katika nganzi ya
Kimataifa, uliandaliwa na Kitengo cha Polisi cha Umoja wa Mataifa (
UNPOL), kitengo ambacho ni sehemu ya Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za
Umoja wa Mataifa, na ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Bw. Jan Eliasson.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi ambayo kwa miaka
kadhaa sasa imekuwa ikitoa Polisi
wake kushiriki katika misheni za ulinzi
wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa, umeongozwa
na Naibu Kamishna wa Polisi na
Mkuu wa Operesheni Maalum Bw. Daniel
Nyambabe.
Akizungumza kwa njia ya video
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki Moon, amesema. “ Kutoka Kabul hadi Kishansa na kutoka Port-au Prince hadi
Pristina, Polisi wa Umoja wa
Mataifa wanatekeleza majukumu yao katika mazingira magumu, hatarishi na
yenye changamoto nyingi. Lakini pamoja na
changamoto hizo bado polisi hawa welevu na mashuja wameendelea kulinda jamii,wanaleta mabadiliko katika maeneo
hayo na mengine mengi kwa kurejesha utawala wa sheria na kufungua
njia za upatikanaji wa usalama na
maendeleo endelevu
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa UN, Jan Eliasson, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
mkutano huo , amewaambia viongozi hao wa Polisi kwamba, kutokana
na changamoto nyingi na kubwa zinazohusu Amani na usalama wa Kimataifa, utekelezaji wa majukumu ya Polisi na kipolisi kuanzia wale wanaohudumu na kushiriki
katika operesheni za Umoja wa
Mataifa, na polisi wote duniani kote unatakiwa kubadilika
na kuwa wa kisasa zaidi.
Maeneo ambayo Polisi wanatakiwa
kubadilika katika utekelezaji wa
majukumu yao ni pamoja na kuwa na
zana na vifaa vya kisasa, uwezo mkubwa na weledi wa hali ya juu katika ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za kiitelejensia, uwezo mkubwa
wa kukabiliana na kwa wakati na mitandao ya kihalifu ya kimataifa ukiwemo ugaidi.
“Kabla ya kumaliza
hotuba yangu, ningepeda
kusisitiza mambo kadhaa ya msingi ambayo ninaamini mtakubaliana nami. Maafisa
wetu ( Polisi) wanatakiwa wawe tayari wakati wowote, wanatakiwa kuwa na
vifaa na zana za kisasa za kazi ,
wanatakiwa wawe wanaopewa mafunzo ya hali ya juu, wanatakiwa wawe na uwezo wa kuwafundisha wengine,
wanaopashwa kuwa na uwezo kuwa na teknolojia za kisasa, wanatakiwa wawe na fursa ya kupata taarifa za kiitelejensia na kuzifanyia
kazi ipasavyo, uwezo wa kupata takwimu
za uhalifu na vifaa vya kuzifanyia uchambuzi takwimu hizo” akasema Eliasson.
Katika kusisitiza hayo, pia ameongeza na kutilia
mkazo nafasi na fursa ya Polisi wanawake ya kushiriki kwa wingi katika misheni za kulinda Amani. Na
kuongeza pia kwamba, maafisa wa polisi wanatakiwa pia wawe ni viongozi wenye uzoefu mkubwa, na wanatakiwa
kuwa tayari kusaidia katika vita dhidi ya
unyanyasaji wa kijinsia na
kingono.
Viongozi wengine waliowazungumza wajumbe hao
ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Operesheni
za Ulinzi wa Amani ( DPKO) Bw. Herve Ladsous pamoja na
Bw. Atul Khare Mkuu wa DFS
Baadhi ya Mada zilizojadiliwa katika mkutano wa wakuu
hao wa Polisi ni pamoja na changamoto za
uhalifu wa kimataifa na Operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, hali ya sasa na ya baadaye kuhusu Polisi waohudumu katika Umoja wa Mataifa pengo,
fursa nafasi na
utaalamu wa Polisi katika Umoja wa Mataifa. Baadhi ya mada hizo zilitolewa na
wataalam kutoka INTEPOL,
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇