Na
Mwandishi Maalum, New York
Umoja
wa Mataifa na Shirika la Afya
Duniani ( WHO), ni baadhi ya Taasisi za Kimataifa ambazo zimeanza kutekeleza kwa vitendo sehemu ya
mapendekezo na ushauri uliotolewa na Jopo la
Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya.
“
Tumeanza kutekeleza baadhi ya mapendekezo ya
Jopo lililokuwa chini ya
Uenyekiti wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe, Jakaya Mrisho Kikwete. Mhe.
Rais nakushukuru sana kwa uongozi wako, ushiriki wako na mchango wako. Nimefarijika kwamba umeweza kuungana nasi
katika mkutano huu kutokea Senegal, kuzungumzia
mapendeko ya Jopo lako”. Akasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Ban
Ki Moon, ameyasema hayo, jana ( jumatatu) wakati wa mkutano
usio rasmi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ulioandaliwa na
Rais wa Baraza hilo, Bw Mogens Lykketoft kwa lengo la kupokea
Ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu uimarishaji na usanifu wa huduma za Afya
Kimataifa: utekelezaji wa mapendekezo ya
Jopo la Ngazi ya juu kuhusu
Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya.
Baadi
ya mambo
ambayo yameanzwa kutekelezwa kwa
mujibu wa Katibu Mkuu yanahusu
Shirika la Afya Duniani ambapo katika
mapendekezo yake, Jopo limeainisha
kutambua kuwa WHO inabaki kuwa
taasisi kiongozi linapokuja suala la afya wakati wote na hususani wakati wa majanga ya dharura ya milipuko ya magonjwa.
“ Jopo
limependekeza kuwa uwezo wa WHO katika kuitika yanapotokea majanga ya dharura ya
kiafya unatakiwa kuimarishwa wakati wote
na kutokana na mapendekezo ya
Jopo WHO imeanzisha mpango wa dharura,
unaokipa chombo hicho uwezo wa
kuwajibika kwa haraka na kwa wakati pale unapotokea mlipuko wa ugonjwa”. Amebainisha Ban Ki Moon.
Pendekezo
la pili mbalo limeanza kufanyiwa kazi na
Umoja wa Mataifa ni lile la
kuimarisha mifumo ya Umoja wa Mataifa hususani wakati wa matukio ya dharura
yanayohusu milipuko ya magonjwa hivyo kuwa na uwajibikaji wa
pamoja kupita Taasisi zake.
“
Tatu nimeridhishwa na hatua ya Banki ya Dunia
ya kuzindua mpango wa dharura wa uwezeshaji wa kifedha pale yanapotokea
majanga ya dharura ya kiafya, ni mpango ambao utatoa uhakika fedha dhidi ya
majanga na utafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na WHO”. Ameeleza
Ban Ki
Moon.
Akielezea
zaidi kuhusu mapendekezo yaliyopendekezwa na Jopo lililoongozwa
na Rais
mstaafu Kikwete. Ban Ki Moon amesema.
“
Mwezi April mwaka jana, niliunda Jopo la
Ngazi ya Juu kuhusu ya Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya ili
litoe mapendekezo ya namna ya
kuimarisha mifumo ya kitaifa na
kimataifa katika kuzuia na kudhibiti
changamoto za majanga ya kiafya katika
siku za baadaye.Mwezi februari mwaka huu,
Jopo liliwasilisha Ripoti yake ikianisha mapendekezo 27 yanayotakiwa kufanyiwa kazi kuanzia ngazi ya taifa,
kanda na kimataifa”.
Mkuu
huyo wa Umoja wa Mataifa, ameyataja baadhi
ya maeneo ambayo yamesisitizwa
na Jopo kuwa ni pamoja na, kuifanya mifumo na miundo mbinu ya utoaji wa huduma za afya kuwa imara
na katika hali ya utayari wakati wote kukabiliana na majanga ya dharura, umuhimu wa tafiti za kisayasi, uhakika wa raslimali
fedha ya kutosha na uwezeshaji kupitia miradi ya maendeleo.
Kwa
mujibu wa Ban Ki Moon, mapendekezo ya Jopo hilo
yamepitiwa kwa uangalifu mkubwa kupitia majadiliano miongoni mwa, na baina ya Taasisi za Umoja wa Mataifa.
Na
baada ya majadiliano hayo, Mkuu huyo wa UM ameandaa taarifa yake ambayo imepewa kichwa cha : Uimarishaji wa Mifumo ya Afya ya Kidunia: Utekelezaji wa Mapendekezoya Jopo la Ngazi
ya Juu kuhusu Mwitikio wa
Kimataifa wa Majanga ya Kiafya.
“
Jopo lililongozwa na Mhe
Kikwete limetupatia mapendekezo ya msingi na yenye tija ambayo kwayo ni kwa namna gani mifumo ya kijamii,
kitaifa na kimataifa itakavyoweza kwa njia sahihi kujiandaa kukabiliana
na majanga ya dharura ya kiafya katika siku
za usoni. Mimi binafsi ninataka kujihusisha kikamilifu katika
utekelezaji wa mapendekezo ya Jopo hili” akasisitiza Katibu Mkuu.
Na katika kuhakikisha kwamba utekelezaji wa
mapendekezo ya Jopo yanasimamiwa na
kufuatiliwa kwa ukaribu, Ban Ki
Moon ameunda Kikundi kazi
kitakachojulikana kama Global
Health Crises Task Force ambacho moja ya majukumu yake makuu yatakuwa ni pamoja na
kufuatilia, ku- ratibu na kuunga mkono utekelezaji wa mapendekezo
ya Jopo.
Kikundi
kazi hicho kitaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw,
Jan Eliasson, Mkurugenzi Mkuu wa WHO. Dr. Margareth Chan, Dr. Jim Yong Kim Rais wa
Banki ya Dunia, na Dr. David Nabarro,
ambaye ni Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu
( Agenda 2030) na Makubalino kuhusu Mabadiliko ya Tabia nchi ( Paris Agreement ).
Kwa upande wake, akiongea kwa njia ya mtandao video ( Video Conference) kutoka nchini Senegal,Mwenyekiti
wa Jopo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho
Kikwete pamoja na kumshukuru, Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa kumkabidhi
jukumu hilo pia alianisha baadhi ya mambo kadhaa ambayo Jopo lake
liligundua wakati wa utekelezaji wa
hadidu za rejea.
Baadhi
ya mambo ni pamoja na, WHO kuchelewa kutamka haraka na kwa wakati kwamba
kuibuka kwa ugonjwa wa Ebola kulikuwa ni
janga la kimataifa na lilotakiwa
kuchukuliwa hatua za haraka
kuzuia maafa yaliyojitokeza.
Kwamba,
WHO haina raslimali fedha jambo ambalo
inabidi itegemee zaidi michango
na hisani za mataifa makubwa.
Kwamba,
nchi nyingi hususani zile zinazoendelea mifumo na
miundo mbinu ya utoaji wa huduma
za afya zikiwamo za afya ya msingi bado ni dhaifu mno kiasi kwamba
kwa vyovyote vile ilishindwa , inashindwa na itashindwa kukabiliana na changamoto
za majanga ya dharura ya
milipuko ya magonjwa kama vile ilivyokuwa kwa Ebola na sasa Zika na tishio la Homa ya
ugonjwa wa manjano.
Rais
Mstaafu Kikwete katika maelezo yake,
amesititiza kwamba, udhaifu huo hauishi katika nchi moja moja bali pia unakwenda hadi ngazi
ya Kikanda na Kimataifa.
“
Jopo letu limegundua kwamba, maisha ya mamilioni ya watu yatakuwa katika hatari kubwa sana na dunia itakuwa katika mashaka makubwa pale
ambapo janga kubwa la
magonjwa ya dharura yatakapoibuka na kukuta mifumo
na miundo mbinu ya utoaji wa huduma za afya haijaimarishwa vya kutosha kukabili changamoto hiyo”.
Amesisitiza Rais Mstaafu
Akaongeza
Kikwete kwa kusema “ Ni matumaini yangu kuwa mapendekezo 27 yaliyotolewa
na Jopo nililoliongoza yatatusaidia
kufika huko tunakotaka kufika. Uungaji mkono wako binafsi Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,
ukichagizwa na utashi wa kisiasa wa viongozi mbalimbali katika ngazi ya juu kadri itakavyowezekana
utasaidia sana katika ufanya mambo yaende”.
Ni
katika kutambua uzito wa dharura itokanayo na magonjwa ya milipuko,
MwenyeKiti wa Jopo Kikwete
amesema Jopo limependekeza pia kwamba kwanza, kuanzishwe Baraza la Ngazi ya Juu Kuhusu Majanga ya Dharura ya Afya ya Jamii, na pili,
kuitishwa kwa Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Majanga ya Kiafya mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇