Na Mwandishi Maalum
Wakati Jumuiya ya Kimataifa ikielekea kukamilisha maandalizi ya Mkutano
Maalum wa Kimataifa kuhusu Masuala ya Kibinadamu, ( World Humanitarian Summit)
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wake, imesema , ni matarajio yake kwamba mkutano huo unatatoka
na makubaliano yanayotekelezeka.
Kauli hiyo
imetolewa siku ya Jumanne , na Balozi
Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, wakati yeye na Mwakilishi wa
Kudumu wa Denmark Balozi Ib Petersen , walipoongoza majadiliano yasiyo rasimi kuhusu uzibaji wa mgawanyiko kati ya mahitaji ya kibinadamu na maendeleo; kutoka nadharia kwenda kwenye
vitendo. Mkutano huo uliandaliwa Mfuko
wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ( UNDP).
“Mkutano ujao ni
fursa nyingine kwa Jumuiya ya Kimataifa ya kuonyesha utashi wa
kisiasa, kujadili kwa kina na tija
changamoto zinazohusu ubinadamu na
misaada ya kibindamu, ni fursa inayotakiwa kutumiwa vema katika utoaji wa
ahadi na utekelezaji wa ahadi hizo kwa vitenda pasipo kumwacha yeyote nyuma”.
Akasema Balozi Manongi.
Na kuongeza kuwa ingawa
Tanzania kama nchi ambayo kwa maiaka
mingi imekuwa ikiwapokea, kuwahifadhi na
kutoa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi kutona nchi jirani, inautizama mkutano huo wa Instambul katika sura mbili tofauti.
Akasema moja ya sababu ambayo
Tanzania inautizama kwa sura tofauti
mkutano huo wa Instambuli kwamba umuhimu unaopewa mkutano huo,
unakizana na umuhimu ambapo nchi kama
Tanzania na nyingine hazikupewa au hazipwewi pale zinapokabiliwa na changamoto kubwa ya kuwawapokea
na kuwahifadhi wakimbizi kutoka
nchi jirani.
“ Tanzania
tumekuwa kwa miaka mingi
tukihifadhi wakimbizi, na katika
miaka ya 90 tulipata changamoto
kubwa sana ya kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi kutoka
nchi jirani, matarijio yalikuwa ni kuona mwitikio wa haraka lakini haikuwa hivyo. Ushirikiano tulioupata ulikuwa wa kutoka Shirika la Wakimbizi la Umoja wa
Mataifa na Nchi za Scandinavia”. Akasema Balozi.
Mkutano wa masuala ya kibinadamu umeitishwa na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki
Moon, utafanyika kati ya 23 na 24
mwezi huu wa March huko Instambul –Uturiki na
unatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi
wakuu wa nchi na Serikali, Taasisi na
Mashirika ya Kimataifa yahusikayo na misaada ya kibinadamu .
Ni mkutano unaofanyika
katika kipindi ambacho pamekuwapo na
wimbi kubwa la maelfu ya wakimbizi wanaokimbia machafuko na vita
katika nchi zao na kukimbilia nchi
za Ulaya kutafuta hifadhi. Huku
mamilioni wengine wakiwa ni wakimbizi wa ndani
au wamekimbilia nchi jirani.
Balozi Manongi,Akabinisha pia kwamba
hata katika Taarifa ya Katibu Mkuu inaonyesha kuwa bado kuna mapengo
katika kughughulikia utoaji wa misaada ya kibinadamu, mapengo
ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi kwa kuanzia kwa watoaji wa misaada,
wasambazaji wa misaada hiyo hadi kwa
walengwa wa misaaada hiyo. Na Akasisitiza
Mkutano huo wa Instambul utatoa nafasi
ya kujitizama upya na angalau kujafa
jambo litakalo weza kuchangia kubadili hali
ya sasa.
Mwakilishi huyo wa Tanzania, amewaeleza washiriki wa mkutano huo, licha ya kufanyika kwa mkutano mbalimbali ya
kimataifa ukiwamo wa 2012
kujadili majanga ya kibinadamu, bado majanga hayo yanaendelea kuwapo
huku ongezeko la hitajio la
misaada ya kibinadamu likiendelea
kuongezeka.
Akaeleza kwamba si kweli kuwa hakuna watu au wadau wenye mapenzi mema na
wanaotaka kusaidia. Bali kinachotakiwa
ni namna gani nchi zinazopata matatizo zinashirikianaje na kwa
pamoja na Umoja wa Mataifa, na wadau mbambali katika kuyakabili matatizo hayo.
Balozi Manongi amebainisha
pia kwamba Tanzania ingepeda
kuona mkutano huo unatoka na
mapendekezo yenye tija ya namna ya kumaliza migogoro na vita na ulinzi wa binadamu
kwa kile alichosema asilimia 80 ya masuala ya kibinadamu na ubinadamu chanzo chake ni migogoro na vita.
Katika mkutano huo ambao Balozi Manongi na Balozi Petersen waliongoza nchi za Ethiopia, Pakistani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo zilielezea uzoefu wao na
changamoto katika kuyakabili majanga ya
kibinadamu yakiwamo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ukame na mafuriko, vita na machafuko na uhifadhi wa wakimbizi
kutoka nchi jirani.
Nchi hizo zilieleza namna
serikali kama zenyewe na kwa ubia na mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo pamoja na wananchi walengwa
ambavyo kwa umoja wao wameweza
kutekeleza sera na mipango ya
kujiandaa kwa maafaa kabla ya hayajatokea, namna zinavyo kabiliana na maafaa hayo yakisha tokea na baada ya
kutokea.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇