Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi
katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani
zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na
viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa
Mshikamano Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya
Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani
Dodoma .
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kombe la ushindi
wa jumla kwa Rais wa TUCTA Gratian Mukoba katika kilele cha Maadhimisho ya
Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Cheti cha Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Ndugu Peter Chisunga katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia namna ya uokozi katika majanga mablimbali yanayotokea Migodini nje ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia jinsi mzani
unavyofanyakazi katika banda la maonesho la Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA nje
ya uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiifurahi picha yake ya
kuchora alipokabidhiwa wakati anakagua mabanda ya Maonesho katika katika kilele
cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniania zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka
kwenye banda la mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii SSRA mjini
Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi OSHA mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanzania TUCTA Ndugu Nicholas Mgaya mara baada ya
kuwasili katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa TUCTA
Gratian Mukoba wakati alipowasili katika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani
Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wazee wa mkoa wa
Dodoma mara baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho hayo ya siku ya
Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na
mamia ya wafanyakazi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Sehemu ndogo ikionesha wafanyakazi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU
.........................
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa
serikali yake itapunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi kutoka asilimia
11 hadi kufikia asilimia 9 kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ili
kupunguza mzigo kwa wafanyakazi.
Rais
Magufuli ametangaza uamuzi huo leo tarehe 01 Mei, 2016 wakati akihutubia katika
sherehe za maadhimisho ya siku ya siku ya wafanyakazi duniani, zilizofanyika
kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
"Napenda
kuwataarifa kuwa serikali yangu kama nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu,
nimeamua kupunguza kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia
9, kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017, nikiwa nina mategemeo makubwa
waheshimiwa wabunge watapitisha bajeti ya serikali niliyoiwasilisha"
Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza
uwanjani hapo.
Pamoja
na uamuzi huo, Rais Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza
kodi katika mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo
ya kuongeza mishahara.
Katika
maadhimisho hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Naibu Spika Dkt. Tulia
Akson, Rais Magufuli amewataka wafanyakazi kote nchini kushiriki kufanikisha
Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma, weledi
na uadilifu.
Amesema
Mpango wa Maendeleo ya Taifa utagharimu takribani shilingi Trilioni 107
zikiwemo shilingi Trilioni 59 kutoka serikalini, hivyo amewataka wafanyakazi
wote kutambua kuwa wanategemewa kuwaongoza watanzania kufanikisha upatikanaji
wa fedha hizo kwa kuchapa kazi.
Aidha,
Rais Magufuli amewataka wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua
wanaozalisha wafanyakazi hewa, huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe
30 Aprili, 2016 jumla ya wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao
kwa mwezi mmoja tu wamelipwa shilingi bilioni 11.6.
"Kwa
hiyo kwa mwaka wafanyakazi hewa hawa wamekuwa wakilipwa shilingi
139,239,285,592.92, ukizidisha kwa miaka mitano kama tungekuwa na wafanyakazi
hewa, miaka mitano tu, tusiseme miaka kumi au ishirini au kumi na ngapi, miaka
mitano tu, manaake wangelipwa shilingi 696,196,427,964.6.
"Hizi
bilioni 696 zinatosha kujenga madaraja kama la Nyerere lililopo Kigamboni,
madaraja matatu, hizi bilioni 696 zinatosha kujenga flyover zinazojengwa Dar es
salaam kwa msaada na mkopo kutoka Japan, zingekuwa saba, hizi bilioni 696
mjiulize kama zingetumika kulipa mishahara ya wafanyakazi waliopo ndani ya
serikali, tungewaongezea mshahara kiasi gani"
amesisitiza Rais Magufuli.
Hata
hivyo Rais Magufuli amewahakikishia wafanyakazi wote ambao wanatekeleza
majukumu yao kihalali kuwa serikali yake itawalinda na kuwatetea huku akitaka
wawapuuze wanaodai serikali ya awamu ya tano haiwapendi wafanyakazi.
"Tukumbuke ya kuwa
kazi ni utu, kazi sio fursa ya kupata mshahara kwa manufaa ya familia zetu bali
ni fursa nzuri ya kutoa mchango kwa taifa lako kwa manufaa ya kizazi cha sasa
na kijacho" amesema Dkt. Magufuli.
You should not just join one site just some instead, that way you have a number of members to choose from.
ReplyDeleteThe internet dating arena has exploded immensely
as increasing numbers of people are depending upon internet to fulfill new people, find
their significant other, friendship and more activities.
By it's very nature, however, online dating sites as you may know it, is
infested with scammers and syndicates, which means you should apply some good sense and
workout a little more caution when joining those hitherto unknown online dating sites websites that every of a sudden spring up and they are boasting of your
veritable collection of Russian women from all of ages and all regions.