China
imekubali kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
reli ya kati yenye urefu wa kilometa 2,561 kwa kiwango cha kisasa yaani
"Standard Gauge" ambao zabuni za ujenzi zinatarajiwa kutangazwa hivi
karibuni.
Balozi
wa China hapa nchini Mheshimiwa Dkt. Lu Youqing ametoa kauli hiyo leo tarehe 25
Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo pia
amemkabidhi barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇