Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa mikoa na wilaya wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ambapo aliwashukuru kwa kazi nzuri waliofanya kipindi cha uchaguzi na kuwataka kuwa wamoja na kukiimarisha Chama.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe.Philip Mangula akizungumza na kutoa neno la shukrani kwa niaba ya Viongozi wote wa CCM waliofanikisha ushindi wa Chama.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akitoa neno la shukran kwa wenyeviti na makatibu wa mikoa pamoja na wilaya walioshiriki kufanikisha ushindi kwa CCM
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza nwa Wenyeviti na Makatibu wa Chama wa mikoa na wilaya wa CCM ambao walioshiriki na kufanikisha ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa kuwashukuru viongozi wa Chama waliofanikisha ushindi kwa CCM.
Baadhi ya Viongozi wa CCM wakinyoosha vidole kutaka kutoa maoni yao kwa Rais Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea Mhe. Albert Mnali akichangia maoni yake kwenye mkutano wa viongozi wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇