Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa
Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi
katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa
Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi
katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na viongozi wengine wakati wimbo wa Jeshi la polisi ukipigwa. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola, Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe , Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yusuph Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu.
Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi
wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
alipokuwa akiwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya
kufungua kikao kazi hicho.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufungua kikao kazi hicho.
Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakiimba Wimbo wa Jeshi la Polisi kabla ya ufunguzi wa Kikao kazi hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na baadhi ya Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa
Upelelezi wa Mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi cha Makamanda wa Polisi,
Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi chao katika ukumbi wa Dodoma Convention Center mjini Dodoma.
.............................
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la
Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza
wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.
Rais
Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao
cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na
Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma
uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.
Awali
kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi
hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu
wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za
kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio
sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.
Kufuatia
kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia
fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa
zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa
likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo
yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.
Ametolea
mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya
kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini
kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya
utendaji kazi kwa jeshi hilo.
"Oysterbay
pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba
mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo
yanafaa. Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia
hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale,
mkaweka investment na Polisi wenu
wakakaa pale. Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia
vibaya nikimaliza mkutano huu,
nataka muelewe na muelewe ukweli direction
ninayoitaka mimi" Amesema Rais Magufuli
Aidha,
Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya mwendesha Mashitaka wa Serikali kujipanga
kufanya kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya
serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria
mahiri.
"Niwaombe
mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi mbele,
kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache,
nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao
wanasema dili limepatikana, na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani
wana-collude Mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu, na wanapo-collude siku zote serikali
inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali inashindwa, halafu siku
hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote serikali inapata kigugumizi"
amesisitiza Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa
zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa
za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.
Hata
hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na
ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo
hivyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇