Na Mwandishi Maalum, New York
Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema, anaimani kubwa
kwamba ushirikiano uliopo
baina ya serikali mbalimbali barani Afrika, mashirika ya kimataifa, makampuni binafsi na kila mtu katika nafasi yake, hapana shaka
ugonjwa wa malaria unaweza kumalizwa
kabisa.
Mhe.
Kikwete ameonyesha matumaini hayo jana(
alhamisi) wakati wa hafla ya kuadhimisha
miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jitihada za
kuutokomeza ugonjwa wa malaria ( Malaria No More) zilizoanzishwa
na Bw. Ray Chambers akishirikiana
na Bw. Peter Chernin.
Katika hafla hiyo na ambayo mshereheshaji alikuwa Bw. Wolf Blitzer
mtangazaji maarufu wa Televisheni ya Kimataifa ya CNN kupitia kipindi chake cha situation Room, Rais mstaafu alitunukiwa tuzo ijulikanayo kama White House Summit Awards ikiwa ni
kutambua uongozi wake, kujitoa kwake
na kubwa zaidi kusimamia uanzishwaji wa muungano wa viongozi wa Afrika
dhidi ya Malaria ( ALMA) muungano ambao
hadi sasa una viongozi 49.
Wengine
waliotunukiwa tuzo hiyo ni Bw. Ray
Chambers na Sumitomo Chemical.
Akijibu
swali la nini anadhani kumechangia katika kupunguza idadi ya vifo
vitokanavyo na ugonjwa wa malaria. Rais mstaafu
amesema, zipo sababu kadhaa, lakini
kubwa ni utashi wa kisiasa wa
kusimamia na kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Akawaeleza
wageni zaidi ya 250 walioalikwa wakiwa ni wawakilishi wa makapuni na mashirika
mbalimbali yanayochongia juhudi za
kuukabili ugonjwa wa malaria. Kwamba, Upatikanaji na usambazani wa dawa sahihi za kutibu ugonjwa
wa malaria, utengenezaji,
usambazaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu na unyunyiziaji wa
dawa za kuuwa mazalia ya mbu ni mambo ya msingi ambayo yamechangia katika kupunguza vifi vya watoto chini ya miaka mitano.
“mchanganyiko
wa mambo hayo matatu umesaidia sana kupunguza idadi ya watoto wanaofariki kwa malaria, lakini pia
matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu ambapo
zaidi ya vyandarua milioni 24.2
vimesambazwa, kumechangia wanafunzi
kuendelea na masomo yao bila kukatishwa mara kwa mara sababu ya malaria,
halikadhalia nguvu kazi imeimarika”. akasisitiza Rais Kikwete na kushangiliwa
na wageni waalikwa.
Akaongeza
kwamba ugonjwa wa malaria unatakiwa kutokomezwa Barani Afrika kwa sababu
unapoteza maisha ya watu wengi, bajeti kubwa katika huduma ya afya inatumika
katika kutibu ugonjwa wa malaria,
lakini uchumi unaathirika kutoka na
nguvu kazi kuugua mara kwa mara.
Akasisitiza “ Malaria inaweza kutokomezwa. Zanzibar
wameweza kutokemeza malaria, mkienda
Zanzibar kutembea msiwe na wasi wasi kupata malaria”. akasema na kushangiliwa
tena na wageni.
kwa upande wake,
Mwanzilishi wa Malaria No More Bw. Ray Chamber, pamoja
na kuelezea historia fupi ya Malaria no more ilikoanzia na ilipofika
na nini mipango ya baadaye. Amemuelezea Rais
Mstaafu Kikwete kama kiongozi
ambaye siyo tu amekuwa mstari wa mbele katika kuukabili ugonjwa wa malaria bali pia amekuwa kiungo muhimu sana
katika mapambano hayo.
“Wakati
nimeanzisha juhudi hizi, nikawa natafuta
mahali pakuwa na center moja na
hasa kwa kuzingatia kwamba Afrika kuna
nchi 43 ambazo zinatatizo kubwa la
malaria, nilikuwa Benin na Mke wangu
tukawa tunajadili pa kuanzia. Nikampigia simu Rais Kikwete na kumweleza
nini nilichokuwa nataka kufanya. Akanijibu haya na tufanye. Sijawahi kuwa na rafiki
kama Rais Kikwete na kwa ushirikiano
wake tumefika hapa” akasema Bw. Chambers na kushangiliwa.
Akabinisha kwa kusema. “Kikwete amekuwa
kiongozi wa kwanza kufanya kazi
nami , kushirikiano wake
alionipa, ushirikiano na wabia
mbalimbali mkiwamo nyingi hapa katika ukumbi huu, Marais wa Marekani, Banki ya Dunia, Global Fund, Bill and Melinda Gates
Foundation, tumeweza kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kwa asilimia 71 na
tumeokoa maisha ya watu wengi.
Bw
Ray Chambers ambaye pia ni mjumbe maalum
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria, anasema katika
miaka kumi ya uhai wa Malaria
no More lengo na mikakati waliyonayo sasa
ni kutokomeza kabisa malaria
ifikapo 2040.
Kwa
upande wake, Mwanzilishi mwenza na Mwenyekiti wa Malaria no More Bw. Peter Chernin,
amesema, katika kuonyesha ni namna gani Rais Mstaafu Kikwete amekuwa mstari wa mbele dhidi
ya ugonjwa wa malaria, alianzisha na
Mama Salma kampeni ya “zinduka Malaria haikubaliki” kwa lengo
la kuwahamasisha wananchi na kutoa elimu
dhidi ya malaria juhudi ambazo zinazaa
matunda.
Akaongeza
kwamba,utashi wa kisiasa upo, utayari
upo, sayansi ipo, nyenzo
zipo, kinachotakiwa ni fedha tu.
Na kwa sababu hiyo akatoa wito kwa wadau wote wenye mapenzi mema kuchangia chochote
walichonacho ili juhudi za kuokoa maisha ya watu wenzi zaidi wakiwamo
watoto iendelee ikiwa ni pamoja na kuitokomeza malaria katika uso wa dunia.
Naye
mwakilishi wa Kampuni ya Sumitomo Chemical,
Bw. Ray Nishimoto pamoja na
kuelezea kazi kubwa iliyofanywa na
kampuni ya A-Z katika kutengeneza vyandarua vyenye viatilifu amesema bila juhudi na ushirikiano
wa karibu aliouonyesha Rais Jakaya Kikwete
kiwanda hicho kisingejengwa Arusha- Tanzania.
Akasema
licha ya kutoa mchango mkubwa katika
kuudhibiti ugonjwa wa malaria Kiwanda cha A-Z kimetoa ajira kwa watu
8,000 asilimia kubwa wakiwa ni wanawake na kwamba Sumitomo Chemical itaendelea na jitihada hizo.
Kikwete akiwa na Bw Blitzer mtangazaji maarufu wa CNN kupitia kipindi chake cha Situation Room
Mwanzilishi wa Malaria no More, Bw Peter Chernin akimkabidhi Mhe. Rais Mstaafu, Kikwete tuzo ya White House Summit Awards ikiwa ni kutambua na kuthamin mchango na uongozi wake katika jitihada za kuukabili ugonjwa wa malaria, wengine waliopewa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Kampuni ya Sumitomo Chemical ambayo imejenga kiwanda cha vyandarua cha A-Z Arusha Tanzania.
Baadhi ya Wageni zaidi ya 250 kutoka masharika na makampuni mbalimbali ambako ni sehemu ya wadau wa kubwa wanaochangia juhudi za kutokomeza na kudhibiti ugonjwa wa malaria
Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielezea juhudi zilizofanywa na serikali ya Tanzania katika kuukabili ugonjwa wa malaria, ilikuwa wakati wa hafla ya miaka 10 ya Malaria no More iliyofayika jjuzi Alhamis New York Marekani, Mhe. Kikwete amealikwa katika hafla hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika pamoja na mengin kuwahamasisha viongozi wa Afrika kuongeza juhudi za kisera, kimkakati na bajeti hali ambayo imechangia sana katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano. pamoja naye ni Bw. Peter Chernin, Bw. Ray Chambers na mwezeshaji, Bw. Wolft Blitzer wa CNN.
Burudani pia ilikuwapo
Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya ya Malaria no More muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇