Msemaji wa CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka
Kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa.
Tuhuma
hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya
wabunge wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale
zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi na kinaunga mkono
jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo.
Lazima
ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi, dini wala kabila, na kwamba
havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa.
CCM
inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua
stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.
Chama
Cha Mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge
wake wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.
Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
31/03/2016
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇