TAARIFA ILIYOSOMWA LEO NA OLE SENDEKA BAADA YA KUTAMBULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO
Machi
15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha
Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi
mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili
waache kukaa kijiweni.
Agizo
hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu
nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa
mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji
mali.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo
lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.
CCM
inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga
kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali
ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
CCM
kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa
na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza
vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi
hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.
Historia
ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa Taifa Mwl.
Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI
baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya Tano inaendesha shughuli
zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo
kila mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.
Utekelezaji
wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirisha katika kipindi kifupi cha uongozi wa
Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa, ufisadi na ubadhirifu
wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na ukwepaji kodi, mambo ambayo
matokeo yake yameshaanza kuonekana.
Matokeo
hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo
yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na umaskini kwa
ustawi wa jamii kwa ujumla.
Aidha
CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na serikali
yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa umma.
Kumbukumbu
zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni pamoja
na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali kwenye
utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria, wamefanyiwa
hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.
Hata
hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa Rais na
serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta na uonevu.
Naomba
ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya uchaguzi ya 2015/2020
kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa hiyo
kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na
ndiyo mahitaji na matakwa ya watanzania walio wengi.
Watanzania
walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na uwajibikaji hivyo
tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri hatua hizi kuwa ni
udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo yao na maneno yao
wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo ambalo CCM haikubaliani nalo.
CCM
inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania wote
kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais Magufuli kwa
dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye Tanzania yenye maendeleo
ifanikiwe.
Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
20/03/2016
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Ole Sendeka akizungumza baada ya kuteuliwa. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Picha: Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Ole Sendeka akizungumza baada ya kuteuliwa. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Picha: Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇