Katibu
Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo akimkabidhi funguo za gari jipya la wagonjwa Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya shughuli ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya
ya Chalinze. Tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokea na kuangalia nyaraka za gari hilo la
kubebea wagonjwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari la kubebea Wagonjwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwasha gari jipya la Wagonjwa lililotolewa na
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili
ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
Sehemu ya Ndani ya gari hilo kama inavyoonekana
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiendesha gari hilo la wagonjwa lililotolewa na
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili
ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
Gari
jipya la Wagonjwa lililotolewa na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya
Hospitali ya Wilaya ya Chalinze kama linavyoonekana kwa nyuma.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia mara baada ya kukabidhiwa Gari hilo la
Wagonjwa.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari na
Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika
picha ni Afisa Usafirishaji wa Ikulu
Athuman Natepe wakwanza kushoto, Mwenyekiti wa Wilaya ya Chalinze Said
Omar Zikatimu wapili kutoka kulia na Dkt. Nasoro Ally Matuzya wakwanza kulia. Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇