Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari na Maelezo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akizungumza mbele ya waandishi wa habari juu ya uamuzi wa serikali wa kulifungia na kulifuta gazeti la Mawio.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti ya kijivu) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia usajili wa Magazeti, Bw. Raphael Hokororo.
Mmoja wa waandishi wa Habari kutoka gazeti la Mwanahalisi akiuliza swali kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kwenye ukumbi wa Idara ya Habari na Maelezo.
Serikali yalifuta Gazeti la MAWIO.
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka
katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.
Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa leo na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati alipokutana na Waandishi
wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo Jijini Dar es
Salaam.
Mhe. Nnauye amesema kuwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa
tarehe 15 Januari, 2016 Serikali imelifuta Gazeti hilo ikiwa ni uamuzi
uliotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).
Alieleza kuwa, hatua ya kulifuta gazeti hilo inazuia pia gazeti la Mawio
kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online
publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura
ya 306.
‘’Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na
mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha
habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa
nchi yetu’’, alisema Nnauye.
Aidha, alifafanua kuwa hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa
baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni,
2013 hadi Januari, 2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina
ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.
‘’Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na Mhariri wa
gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa
gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti,
Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari
kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo
zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba
inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za
nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo’’ alisisitiza Mhe.
Nnauye.
Katika hatua nyingine, Waziri nape alitoa pongezi kwa Vyombo vyote vya
habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma
ya habari na sheria nyingine za nchi.
‘’Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa
vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na
kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja na wahariri wa magazeti ya; Mwananchi
Tanzania, Mtanzania, The East African, Magazeti ya Daily News na Habari Leo, Uhuru
na mengineyo’’, alisema Mhe. Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti ya kijivu) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia usajili wa Magazeti, Bw. Raphael Hokororo.
Mmoja wa waandishi wa Habari kutoka gazeti la Mwanahalisi akiuliza swali kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kwenye ukumbi wa Idara ya Habari na Maelezo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇