RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisjo Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na watoto watatu wa marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman, aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini, TAA, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, leo Januari 19, 2016 kutoa mkono wa pole. Marehemu Suleiman alifariki Jumatatu Januari 18, 2016 wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi na tayari amezikwa. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
RAIS
mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo Januari 19, 2016 amehani
msiba wa aliyekuwa Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini,
marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman.
Dkt.
Kikwete aliwasili nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, akifuatana
na mkewe Mama Salma Kikwete majira ya saa 10;30, akitokea kijijini kake Msoga
mkoani Pwani.
Baada
ya kiwasili, nyumbani kwa marehemu Rais mstaafu alipokewa na mdogo wa marehemu,
Mhandisi, Nasiri Said Suleiman, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Laurent Mwigune, Mkurugenzi wa Sheria na
Mawasiliano ya umma, Bw. Ramadhan Maleta, maafisa wa TAA, na wanafamilia
wengine na kwenda moja kwa moja kuweka saini kitabu cha maombolezo.
Baada
ya kufanya mazungumzo kwa muda, Watoto wawili wa marehemu ambao wanasoma nje ya
nchi nao waliwasili na kupata fursa ya kusalimiana na Rais mstaafu, Dkt.
Kikwete.
Watoto
hao ni pamoja na motto mkubwa wa marehemu, Mohammed Said Suleiman, na mdogo
wake Said Suleiman Said.
Baadaye
Rais alikwenda kusaliamiana na mama mzazi wa marehemu, mke wa marehemu na
wafiwa wengine na kasha yeye an msafara wake kuondoka majira ya saa 11 jioni.
Mhandisi
Suleiman Said Suleima, alifariki dunia Januari 18, 2016 majira ya asubuhi
wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi katikati ya Magogoni
na Kigamboni na kuzikwa jioni ya siku hiyo hiyo.
Marehemu
ameacha mjane na watoto watatu, Mohammed, Said na Hosam.
Akisaini kitabu cha maombolezo
JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Bw. Ramadhan Maleta
JK akimpa pole mtoto wa mwishi wa marehemu, Hosam Suleiman Said Suleiman
JK akimpa pole mtoto mkubwa wa marehemu, Moahmmed Suleiman Said Suleiman
JK akimsikiliza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, TAA, Bw.Laurent Mwigune
JK akisalimiana na mdogo wa marehemu, Mhandisi Nasiri Said Suleiman
JK akimpa pole mama wa marehemu
Mama Salma Kikwete, akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Suleiman Said, baada ya kuhani msiba wake Januari 19, 2016
JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Kazi Maalum wa TAA, Mhandis Thomas Junior Haule
JK akisalimiana na Meneja Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mohamed R.Ally
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇