LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2015

MWENYEKITI WA CCM TAIFA AWASILI DODOMA TAYARI KUONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kwenye uwanja wa Ndege wa  muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma tayari kwa kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikweteakisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma tayari kwa kuongoza kikao cha  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbali mbali wa CCM mkoa wa Dodoma waliojitokeza kumpokea, Mwenye kiti wa CCM  ataongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa  kitakachojadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages