Rais Magufuli, aliwashukuru wananchi kwa mara nyingine kwa kumuamini na kumchagua, ambapo ameahidi kuwa kiongozi atakayewatumikia watu wote bila kubagua, na kwamba lengo lake ni kuhakikisha nchi ya tanzania inasonga mbele kimaendeleo.
Rais Magufuli kwenye hotuba yake pia akaeleza malalamiko aliyoyapokea kwa wananchi ambayo yeye anaona ni kero kwa wananchi, maeneo ambayo anasema ni lazima yashughulikiwe ipasavyo ili kuleta uaminifu kwa wananchi.
Kuhusu Uchumi rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itakuwa ni serikali ya viwanda itakayosimamia sheria na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unasimama kwa kujenga na kuendelea viwanda ili kutengeneza ajira zaidi.
katika hotuba yake pia, rais magufuli hakuacha kugusia suala la katiba mpya, ambapo amesema atahakikisha serikali yake inasimamia mchakato huo na kwamba safari hii utakamilika kwa wakati.
Rais Magufuli pia akagusia suala la Muungano pamoja na hali ya kisiasa visiwani zanzibar ambapo amesema yeye ni muumini mkubwa wa muungano uliopo na kwamba anaamini mgogoro wa Zanzibar uliojtokeza unatatuliwa kwa amani.
Kabla ya kuanza kwa hotuba yake bungeni, rais Magufuli alishuhudia vioja vya upinzani ambao walikuwa wakipiga kelele wakati viongozi wa zanzibar walipokuwa wakiingia bungeni bungeni, ambapo baadae spika wa bunge Job Ndugai alilazimika kutumia kiti chake kuwafukuza nje ya ukumbi wa bunge ili kupisha hotuba ya rais kuanza, jambo ambalo upinzani ulitii na kutoka nje.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇