LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2015

MTEMVU AVUNA WANACHAMA 75 TOKA VYAMA VYA UPINZANI DAR ES SALAAM



  Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Temeke kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Abbas Mtemvu, akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Keko eneo la Kachimbe Ubungo,  Dar es Salaa jana


Katibu Mwenezi wa Jimbo la Temeke, Ali Kamtande akihutubia jukwaani
Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Hassan Kitigi akizungumza na wananchi na wanachama hao

Wananchi na wanachama wakimsikiliza Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu




Mama mtemvu akisalimia wananchi na wanachama wakati wa Mkutano huo na kumuombea kura Mgombea nafani ya Urais ,Udiwani na kumuombea mumuwake


Mgombea Ubunge kura za maoni CCM 2015, Arnold Mushi akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano uliofanyika katika Kata ya Keko eneo la Kachimbe Ubungo,  Dar es Salaa jana .




MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu amesema amejipanga vizuri kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa miaka mitano mingine iwapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo.

Mtemvu alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika jana katika Kata ya Keko eneo la Kachimbe Umbungo jijini Dar es Salaam.

"Serikali na chama chetu cha CCM tuna mipango ya maendeleo ya miaka mitano tuliyoindaa tunaomba mtuchague tuweze kuikamalisha" alisema Mtemvu.

Alisema wakazi wa eneo hilo wasiwe na wasiwasi wowote wala kuyumbishwa kwani kunafedha sh. bilioni 14  kwa ajili ya shughuli za maendeleo na uboreshaji wa miundombinu .

Mtemvu alisema hivi sasa wamejiandaa kujenga barabara za kiwango cha lami katika mitaa kadhaa ya Keko ambazo zitawekwa taa za sola.

Aliongeza  kwa kipindi ambacho walikuwa katika uongozi wamefanikiwa kujenga miundombinu ya barabara, kuweka taa na kujenga shule za sekondary mbili kati ya hizo zikiwa na kidato cha tano na sita pamoja na kuhimarisha kwa huduma za afya kwa kujenga zahanati jambo ambalo ni la kujivunia.

Mtemvu aliwaomba wananchi hao na makada wa CCM katika nafasi ya urais wampe kura Dk. John Magufuli, Ubunge wampe yeye na udiwani wampe Francis Mtawa ili mambo yaende sawa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages