Na Mwandishi Maalum, New York.
Wakati majukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ( ICTR) yakifikia ukingoni mwishoni mwa mwaka huu, hatima ya wafungwa waliomaliza vifungo vyao na wale walioachiwa huru bado haijajulikana.
Wakiwasilisha kwa nyakati tofauti mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya jumanne, Taarifa ya (ICTR) na Taarifa ya Taasisi ya Kimataifa itakayo hifadhi nyaraka na kumbukumbu zote zinazohusiana na mahakama hiyo (IRM) Marais wa vyombo hivyo, Jaji Vagn Joesen na Jaji Theodor Meron wamesema, mahali pa kuwapeleka waliomaliza vifungo na walioachiwa bado ni changamoto kubwa.
Marais hao ambao mmoja ( Jaji Joesen)alikuwa akiwasilisha taarifa yake ya mwisho kwa upande wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbali ya Rwanda ,wamepongeza Mhe Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na watanzania kwa kuwa mwenyeji wa ICTR kwa miongo miwili ya uhai wake.
Akasema Jaji Theodor Meron “ Mwezi Julai mwaka huu, tuliweka jiwe la msingi la makazi mapya yakayoiridhi ICTR, uwepo wa Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwenye hafla hiyo ni udhihirisho wa namna gani Tanzania imekuwa ikishirikiana na ICTR katika utekelezaji wa majukumu yake kuanzia ilipoanza, inapoishia na inakoelekea katika majukumu hake mapya.”
Akaongeza kuwa ujenzi wa makazi hayo mapya na ambayo yanajengwa katika eneo la Laki Laki katika jijini la Arusha, unaendelea vema na kwamba nyaraka na kumbukumbu zote muhimu za ICTR zitakuwa na mahali salama pa kuzihifadhi na vikiwamo pia vyumba vya mahakama kwaajili ya kumaliza kesi za masalia.
Akasema Taasisi hiyo ya Kimataifa inayochukua nafasi ya ICTR imejianda vema katika kutekeleza majukumu yaliyombele yake na makabidhiano yanaendelea vema.
Akizungumzia kuhusu mahali pa kwenda wafungwa waliomaliza vifungo vyao na ambazo mahakama iliwaachia, Jaji Meron ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kutoa ushirikiano katika kusaidia upatikanaji wa makazi mapya kwa watu hao.
Akasema wafungwa waliomaliza vifungo vyao na kuachiwa wanaogopa kurudi kwenye nchi yao kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
Ombi jingine ambalo Jaji Meroe amelitoa mbele ya Umoja wa Mataifa ni pamoja na lile la kukamatwa kwa watuhumia ambao wapo mafichoni ili waweze kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.
Viongozi hao wamesema wao binfasi wamejifunza mengi kutokana na ushiriki wao katika utekelezaji wa kusimamia haki huku wakisisitiza kuwa katika uhai wake ICTR siyo tu imekuwa chombo cha kutoa haki lakini pia chombo ambacho watu kutoka mataifa mbalimbali na kada tofauti wakiwamo wanafunzi wa Vyuo Vikuu wamekutumia chombo hicho kama mahali pa kujifunza , kujielimisha na kujibaharisha.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,pamoja na kuwashukuru Marais hao kwa utekelezaji wa majukumu yao na kusimamia uanzishwaji wa Taasisi zitakazoridhi kazi za mahakama ya ICTR na ICTY naye amesisiza haja na umuhimu wa jumuiya ya kimataifa wa kuwachukua wafungwa waliomaliza vifungo vyao.
Vile vile Balozi Tuvako Manongi amesema wakati Tanzania ikiendelea na kujianda kuwa mwenyeji wa IRM, ingependa kuona kwamba gharama ambazo si za lazima za uendeshaji wa matawi mawili yanayochukua nafasi ya ICTR ambalo liko Tanzania na ICTY ambalo liko the Hague linazingatiwa.
Your Ad Spot
Oct 14, 2015
Home
Unlabelled
MARAIS WA MAHAKAMA ZA KIMATAIFA ZA MAUAJI YA KIMBARI WAMPONGEA JK, TANZANIA KWA USHIRIKIANO
MARAIS WA MAHAKAMA ZA KIMATAIFA ZA MAUAJI YA KIMBARI WAMPONGEA JK, TANZANIA KWA USHIRIKIANO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇