Mkutano wa Nne unaowakutanisha Maspika 180 na Manaibu Spika 35 kutoka nchi 140, unaanza leo ( jumatatu) hapa Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa.
Mkutano huu wa siku tatu na ambao umeandaliwa na Chama cha Mabunge Duniani ( IPU), utafunguliwa na Rais wa IPU Bw. Chowdhury Saber na Katibu Mkuu wa Umoja wa Matafa, Ban Ki Moon.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu. Mkutano ambao Maspika wanatarajiwa kujadiliana kwa kina namna ya kukabiliana na changamoto za Amani, Demokrasia na Maendeleo kwa maono ya Kibunge.
Mkutano wa Nne wa Maspika, ulitanguliwa na Mkutano wa Kumi wa Maspika wanawake, mkutano uliofanyika kwa siku mbili ( jumamosi na Jumapili). Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda ameshiriki kikamilifu na kuongoza baadhi ya mikutano.
Mkutano wa Nne wa Maspika ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya Maspika hao na ambayo imekuwa ikifanyika kuelekea Mkutano wa Kilele wa Viongozi wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika wiki chache zijazo ambapo watapokea na kupitisha Ajenda Mpya za Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Kumi wa Maspika wanawake, mkutano uliojadili mbinu za kuchagiza usawa wa kijinsia, miaka 20 baada ya Beijing pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa malengo 17 ya Maendeleo Endelevu Baada ya 2015.
Maspika
Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa IPU Bw. Choedhury
Saber na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Martin Chungong wakati wa mkutano wao
wa siku mbili uliofanyika jumamosi na jumapili, ukitangulia mkutano wa
nne wa Maspika wa Mabunge
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇