TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Siku za hivi
karibuni kumeibuka baadhi ya watu ambao wamekuwa kwa makusudi na kwa malengo
maalum wakitunga na kujiandikia taarifa, za uongo, kujenga hofu na au kupotosha
na kisha kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa malengo mahsusi
dhidi ya Chama Cha Mapinduzi.
Watu hao katika
nyakati tofauti wamekuwa wakitengeneza uzushi na uongo huo na kuusambaza kwenye
mitandao pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kwa lengo lisilo wazi.
Baadhi ya uzushi na
uongo uliotungwa na kusambazwa na watu au kikundi hicho ni pamoja na hii ya leo
inayoeleza mambo mbalimbali juu ya Ndugu Edward Lowasa na ambayo watunzi wake
wameandika kuwa imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses
Nnauye.
Ifahamike kuwa
uzushi huo na mwingine uliofanywa na watu au kikundi hicho umekusudia kujenga
msukumo ambao haupo ili kuujengea umma hofu ya huruma dhidi yao ili kusukuma na
kushinikiza agenda zao.
Jambo hilo ni uzushi
mtupu kwa sababu kwanza Ndugu Nape na wajumbe wote wa Sekretarieti hawapo
jijini Dar es Salaam badala yake wapo mikoani kushiriki katika zoezi la kura ya
maoni kwa ajili ya uteuzi wa wagombea Udiwani na Ubunge zoezi ambalo
litakamilika Agosti Mosi, 2015.
CCM inasisitiza kuwa
habari hizo si za kweli, zimeandikwa na watu kwa malengo binafsi ya kugombanisha,
kujenga chuki na uhasama baina ya Ndugu Nape, Chama, Wajumbe wa Sekretarieti na
wananchi kwa ujumla bila sababu.
Viongozi, wana-CCM
na wananchi kwa ujumla hawana budi kupuuza uzushi wowote ule unaotolewa na
kusambazwa na watu au vikundi vya hovyo vinavyotumiwa na watu kwa maslahi
binafsi, badala yake CCM itakuwa inatoa taarifa sahihi kwa wakati ili
kutoruhusu uwepo au kuibuka kwa ombwe la mawasiliano baina ya umma na Chama.
Imetolewa na:-
Kitengo cha
Mawasiliano na Umma
Ofisi Ndogo
ya Makao Makuu ya CCM
Lumumba, Dar
es Salaam.
29/07/2015
By by ccm. ..mwaka huu ndo mwisho wenu
ReplyDeleteBy by ccm. ..mwaka huu ndo mwisho wenu
ReplyDelete