Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Sita tangu Wilaya ya Iramba
ianzishwe,amepokea Kijiti cha Ubunge Mwaka 2010 kutoka kwa Aliyekuwa
Mbunge Ndugu.Kirimba.Mara baada ya kuchukua Ubunge wa Iramba ,Mwigulu
Nchemba amebadilisha sura ya maendeleo ya Jimbo hilo katika maeneo ya
Fuatayo.
Mwigulu
Nchemba wakati akiingia kuwa Mbunge wa Iramba alikuta Wilaya inaumeme
maeneo ya Tarafa tu,Kata na Vijiji vilikuwa havina Umeme.Hivi sasa
Mwigulu Nchemba amefanikiwa kuwasha umeme katika kata zote na Vijiji 48
vya Jimbo Zima.Hii haikuwahi fanyika kabla ya Mwigulu kuwa Mbunge wa
Iramba.
Mbali na
Umeme,Mwigulu Nchemba akitambua shida ya Maji inayolikumba jimbo
lake,Amefanikiwa kufungua miradi 8 ya Maji katika Kata ya
Ndago,Shelui,Mgongo,Kyengege, KInapanda n.k Wakati huo vijiji Zaidi
ya 62 hivi sasa visima vinachimbwa ilikufanikisha huduma kwa Wananchi
wake.Pia ujenzi wa barabara za ndani ya Jimbo na hata za kuunganisha na
wilaya zingine zimeimarishwa na hata kupandishwa daraja kuwa chini ya
TANROADS.
Kwa
maendeleo hayo na mengine kama Kusomesha watoto wa familia zisizojiweza
Zaidi ya 200,Kusambaza vitabu kwa kila shule vyenye thamani ya
Tsh.Milion 7 kwa kila shule.Pia amekwenda mbali zaidi amekuwa Mbunge wa
Kwanza kusambaza dawati 200 kwa kila shule ya Jimbo lake na Mbunge pekee
aliyechangia Mifuko zaidi ya 100 kwa kila shule kwaajili ya Ujenzi wa
maabara pamoja na Flame zake za Madirisha na Milango.
Maendeleo
yote haya ambayo hayakuwahi kufanywa na wabunge waliopita kunampatia
nafasi kubwa sana Mwigulu Nchemba kuendelea kuwatumikia wananchi wa
Iramba,Kwa Taasisi za Kidini amekuwa mstari wa mbele kujenda na Kufunika
Makanisa na Misikiti mbalimbali ndani ya Jimbo lake.
Wananchi wa Iramba hii leo wamejumuika naye kuhakikisha anakamilisha hatua zote za ndani ya Chama na taratibu za Uchaguzi ili tar.25/10/2015 aweze kuchaguliwa tena kuwaongoza.
Wananchi wa Iramba hii leo wamejumuika naye kuhakikisha anakamilisha hatua zote za ndani ya Chama na taratibu za Uchaguzi ili tar.25/10/2015 aweze kuchaguliwa tena kuwaongoza.
Mwigulu
Nchemba anaandika historia ya pekee kuwa Mbunge wa Iramba mwaka
2010,Mwaka 2011 aliteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Mh;Jakaya Mrisho
kikwete kuwa Mtunza hazina ya CCM Taifa,Mwaka 2012 Mwigulu anachaguliwa
tena kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara ikiwa ndio mara ya
kwanza CCM inakuwa na Kiongozi Mkubwa(Top 4) mwenye Umri chini ya miaka
40.
Mwaka 2013
Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha anayehudumia
Sera.Mtiririko huu wa Uongozi na kwa kuzingatia namna alivyokuwa mstari
wa mbele kusimamia maslahi ya Watanzania wote (wanyonge na Masikini) na
hatiye kujitosa kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano.Mwigulu Nchemba
anaonekana ni TAA mbele ya Wanairamba na hivyo wamekuwa wakisisitiza
kuwa ndiye chaguo lao na Wanaimani naye kubwa kuwa atawasadia katika
kupandisha shughuli za maendeleo yao.
Kauli mbiu ya Mwigulu iliyoshika kasi Nchini kwa sasa ni "MABADILIKO NI VITENDO NA WAKATI WAKE NI SASA"
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇