Wandesha bodaboda wakiwa wamejipanga kwenye eneo la mapokezi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Bukoba Vijijini kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana kwa furaha na Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini, Profesa anna Tibaijuka, wakati wa mapokezi yake kuingia wilaya ya Bukoba Vijijini leo, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa iani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Kagera, leo.
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akimuaga, Kada wa CCM, Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongela, wakati wa mapokezi ya Kinana, kuingia wilaya ya Bukoba vijijini leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Mjumbe wa NEC, ambaye mewahi pia Katibu wa CCM mkoa wa Kagera, Mzee Justine Kamaleki, wakati wa mapokezi ya Kinana kuingia katika wilaya ya Bukoba Vijijini leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia ukumbi wa Bandari, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Bukoba Vijijini, tayari kwa kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini leo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bukoba Vijijini, akitoa utangulizi kumkaribisha kuzungumza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika kikao hicho cha ndani. Kushoto ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza na Mjumbe wa NEC, Nazir Karamagi
Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba Vijijini akisoma taarifa ya wilaya hiyo wakati wa kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Kinana kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Kada wa CCM , Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini, Jakson Msome akisalimia baada ya kutambuliwa na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera (kulia)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye Kikao hicho kabla ya kuendelea na ziara yake katika wilaya ya Bukoba Vijijini leo. Kinana amewataka viongozi wote kutokuwa na wagombea wao mioyoni katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, pia amewataka wapambe wa viongozi kuacha umbea wa kuuza maneno kutoka huku kwenda kule kwa sababu hali hiyo ni chanzo cha fitina miongozi mwa viongozi na wanachama
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi cheti cha CCM, mhitimu katika Chuo Kikuu cha St. Augustine, Amosi Joseph, wakati wa mkutano huo, leo. Jumla ya wahitimu 120 ambao ni wanachama wa CCM walitunukiwa vyeti hivyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufukia mtaro wa bomba la maji, alipokagua ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Ibwera, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera, leo
Katibu wa Mradi huo wa Maji, Hassan Omar akimweleza Kinana malalamiko ya wanajiji hicho cha Ibwera kuhusiana na mradi wa maji wa kijiji hicho kuchelewa kukamilika ambapo kwa mujibu wa barua aliyomuonyesha kutoka kwa wasimamizi wa mradi huo, ulipasw auwe umekamilika tangu mwaka jana.
Wananchi wa Kijiji cha Rukoma, wakitangulia mbele ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Katibu Mkuu huyo alipowasili katika kijiji hicho leo, kufungua tawi lao la CCM na kufanya mkutano wa hadhara, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM akiwasili kwenye Ofisi mpya ya CCM katika Kijiji cha Rukoma, tayari kwa kuizindua leo.
Vijana wa kijiji cha Rukoma wakiwa na furaha ya aina yake wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akizindua rasmi Ofisi ya CCM ya Kijiji hicho leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Ofisi ya CCM ya Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia katika Ofisi hiyo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jason Rweikiza wakitoka katika Ofisi hiyo.
Kijana akiwa amekwea mti kuhakikisha anamuona Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati anahutubia Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuhutubia mkutano huo katika kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini leo
Mbunge wa Bukoba Vijijini Jason Rweikiza akieleza mchango wake aliofanya katika utekelezaji wa ilani ya CCM wakati wa mkutano huo wa Kinana katika Kijij cha Rukoma leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kijiji cha Rukoma, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi baada ya kumaliza hituba yake katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsikiliza kijana ambaye ni mkulima wa kahawa, baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake katika Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera. Kijana huyo alimweleza kuhusu changamoto wanazopambana nazo wakuliza wa zao hilo husuasan bei ndogo.
Wananchi wa Kijiji cha Katoro wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera, wakimshangilia Kinana alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo
Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela akizungumzana wananchi katika mkutano huo wa Kinana uliofanyika Kijiji cha Katoro. Mongela amewataka wananchi wote kujiandiksha katika daftari la kudumu la wapigakura, lakini kuwa macho na wageni kutoka nchi jirani ambao baadhi yao wamekuwa wakijaribu kujiandikisha katika daftari hilo, kinyume cha sheria
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo katika Kijiji cha Katoro, wilaya ya Bukoba Vijijini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Katoro wilaya ya Bukoba Vijijini leo |
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Sheikh Mustafa Khalid Sudi baada ya kumaliza kuhutbia wakazi wa kata ya Katoro wilaya ya Bukoba Vijijini |
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jason Rweikiza wakishikana mikono na makatibu wa CCM waliopo Kata za jimbo hilo, kama ishara ya Katibu Mkuu huyo kuwakabidhi baiskeli makatibu hao, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Katoro wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera leo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape NNauye, akizama umati wa wapenzi na wanachama wa CCM wa kata ya Katoro wanavyoondoka baada ya kumalizika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika kijiji hicho leo. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇