Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi
wa habar katika ofisi za CCM makao makuu jijini Dar es salaam wakati
akizungumzia kusogezwa mbele kwa vikoa vya Halmashauri Kuu na Kamati
Kuu.(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………………………………….
Chama cha Mapinduzi kinatarajia kufanya vikao vyake mjini Dodoma ambapo tarehe 22 Mei kitafanyika kikao cha Kamati Kuu ya CCM ambapo tarehe 23 na 24 kutakuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam,Katibu wa Nec,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,amesema sababu
ya kuahirisha vikao hivyo ni kupisha ratiba ya vikao vya baraza la
wawakilishi vitakavyoanza Mei 18 mwaka huu.
”Vikao vya baraza la wawakilishi vitaanza Mei 18 hadi 21,vikao
hivi ambavyo vitafanyika mfululizo vitatoa ratiba ya wagombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais wa Zanzibar,Wabunge na Baraza la
Uwakilishi,”amesema Nape
Nape alisema ratiba hiyo itawezesha wagombea kujitangaza na kuchukua fomu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇