Wakati hali ya kisiasa na kiusalama
ikiendelea kuwa ya sintofahamu Nchini Burundi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki Moon, ameelezea kutiwa moyo na juhudi mbambali zinazolenga kurejesha
hali ya amani na usalama nchi humo.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu, siku ya Ijumaa hapa Umoja wa Mataifa, imesema,
katibu Mkuu anatiwa moyo na
juhudi zinazofanywa na makundi mbalimbali
ya kikanda, ya kidini, ya
kijamii, vyama vya siasa pamoja na Mwakilishi Wake Maalum katika Eneo la Maziwa Makuu katika kuhakikisha kwamba
mgogoro na sitofahamu iliyoikumba
Burundi inatafutiwa ufumbuzi.
Wahusika wakuu ambao Ban Ki Moon ameelezea kutiwa moyo na juhudi zao za
kuleta amani nchini Burundi ni pamoja na
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo ipo chini ya uenyekiti wa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Umoja wa
Afrika ( AU), Soko la pamoja la
Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ( COMESA),
Mkutano wa Kimataifa wa Eneo la Maziwa Makuu ( ICGLR) na
Mwakilishi wake Maalum katika eneo la
maziwa Makuu Bw. Said Djinnit.
“ Katibu Mkuu anawapongea washirika
wote wanaoshiriki mchakato huo pamoja na
mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa, hususani katika kupunguza hali ya wasiwasi na sintofahamu
na kujenga mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi huru, wa haki, jumuishi na wa amani.” Inasomeka Taarifa ya katibu Mkuu.
Hata hiyo pamoja na kutiwa moyo
na kazi nzuri inayoendelea
kufanyika, Katibu Mkuu ameelezea wasi wasi wake hali mbaya ya kibinadamu inayowakabiri wakimbizi kutoka Burundi ambao wamekimbilia nchi za jirani ikiwamo
Tanzania.
Pamoja na wasiwasi huo Ban Ki
Moon amezipongeza nchi jirani
kwa kutoa misaada ya kibinadamu ikiwa ni
pamoja na kuwahifadhi wakimbizi
hao. Huku akitoa wito kwa Serikali ya
Burundi kuandaa mazingira ya kuwarejesha nchi humo raia wake waliokimbia
machafuko.
Vile vile Katibu Mkuuu, amewahimiza wadau mbalimbali kuendelea na majadiliano kwa lengo la kufikia makubaliano ya jumla katika maeneo yote ambayo wameyaainisha. Huku akithibitisha utayari wa
Umoja wa Mataifa katika kuwasaidia wananchi wa Burundi na Kanda kwa ujumla katika mchakato huu.
Taarifa kutoka Mashiri kaya Kimataifa likiwa mola wakimbizi, UNHCR
zinazonyesha kwamba tangu mwezi April imwaka huu, jumla ya wananchi 100,000 wa Burundi
wakimbia nchi yao na kuvuka mipaka nakuingia katika nchiza Tanzania, Rwanda
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wimbihilo la wakimbizi,
limesababisha kuibuka kwaugonjwa wa kipindupindu katika kambi iliyoko Kigoma ugonjwa ambao umesabisha vifovyawatu
37 kwamujibuwa UNHCR na kwamba Serikali ya
Tanzania imekwishakutangaza uwepo wa ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇