Burudani ikitolewa kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa |
wahitimu |
Burudani ikitolewa na baadhi ya wanafunzi katika mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa |
hapo sasa viduku kwenda mbele |
Maombi kwa wahitimu |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
WAHITIMU katika shule za sekondari nchini
wameshauriwa kuviendeleza vipaji vya sanaa wanavyoonesha kwenye sherehe
mbalimbali wakiwa shuleni wakitambua kuwa vina mchango mkubwa katika kuwapa
ajira maishani mwao.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna alitoa ushauri huo kwenye mahafali ya
kidini ya Ukwasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya
sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa.
Kajuna alitoa ushauri huo baada ya kukunwa na vipaji
mbalimbali vya sanaa walivyoonesha wahitimu na wanafunzi wanaobaki kama
ilivyowafurahisha pia waalikwa wengine ukumbini hapo.
Miongoni mwa vipaji vilivyooneshwa na wanafunzi wa
shule hiyo ni pamoja na uimbaji wa nyimbo za injili uliodhihirisha kwa kiasi
kikubwa wanafunzi hao wanao uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba tenzi na mashairi
ya nyimbo mbalimbali.
Sanaa nyingine ni uchezaji wa aina mbalimbali wa
nyimbo za injili,Uongozaji wa sherehe,uchekeshaji na upigaji wa vyombo vya
muziki zikiwemo ngoma na kinanda.
Kajuna alisema si wakati tena kwa wanafunzi kuacha
sanaa hizo zikaishia mashuleni,badala yake wahakikishe wanaziendeleza hata
wafikapo katika vyuo na baadaye wazifanyie kazi katika kuwapa ajira badala ya
kubaki wakitegemea kuajiriwa pekee.
“Kama mna vipaji kama mlivyoonesha hapa sidhani kama
mnapaswa kuwa miongoni mwa watanzania ambao katika miaka kadhaa ijayo
watatakiwa watembee kutwa nzima na bahasha za kaki wakipita kila ofisi kuomba
kazi.Unatembea mchana kutwa mpaka bahasha inachanika upande wa juu.Uliiweka
kiganjani baadae unaamua uiweke kwapani”
“Tumieni vipaji vya sanaa mliyoonesha hapa kujiajiri
katika miaka hiyo.Huu ni utajiri tosha unaoweza kuwapa maisha bora tena pasipo
kutumia gharama kubwa kama ilivyo kwa wengine.Mmeonesha mnaweza” alisisitiza
mwenyekiti huyo wa uvccm mkoa.
Hata hivyo Kajuna alisema mchango wa wazazi,walezi
na wadau wengie ndiyo msingi mkubwa katika kuendeleza vipaji vya sanaa walivyo
navyo wanafunzi hivyo akawaasa kutambua vipaji wal;ivyonavyo watoto wao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇